Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's akizungumza na waandishi wa habarin (hawapo pichani) juu ya tamasha la pasaka litakalofanyika Machi 27 katika viwanja vya leadar's jijini Dar es Salaam,katika ni Maneja Uendeshaji, Shaweji Steven, Kushoto ni Meneja wa Gospel, Emmanuel Mweta.
02.Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's wakati akitangaza tamasha la pasaka la Machi 27 mwaka huu leo jijini Dar es Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)
Na Chalila Kibuda, Globu
ya Jamii
UPENDO Music Festival
imeandaa tamasha la Injili litakalofanyika Machi 27 mwaka huu katika
viwanja vya Leader,s jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi
habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International,
Amarido Charle's amesema kuwa tamasha hilo litakuwa na ubora
kutokana na walivyoliandaa kwa miaka mingi na sasa imetimia waumini mbalimbali
kuungana kuikaribisha pasaka.
Charle's amesema kuwa
tamasha litakuwa na vionjo mbalimbali kutoka kwa wasanii wa injili katika wa
vikundi mbalimbali bila kujali kanisa analotaka.
Amesema wamekuja katika
tamasha kwa muonekano tofauti kwa wasanii kutumia majukwa tamasha hilo
kujitangaza na sio kupigiwa simu hali hiyo ndio imesaidia nchi zilizoendelea
kuwa na wasanii nyota kutokana na kujitoa katika matamasha.
Tamasha hilo litakuwa na
viingilio ikiwa kama sehemu ya uendeshaji wa uwanja na sio kwa ajili ya
kujinufaisha kwa kuwa na kiingilio kwa mkubwa sh.5,000 na viti maalum kwa
sh.10,000.
Charle's amesema kuwa
kuanzia majira saa nne kutakuwa na michezo mbalimbali katika viwanja hivyo nia
ikiwa na kutambua na vipaji vingine vya michezo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...