KUELEKEA siku ya wanawake duniani wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water front jijini Dar es Salaam leo wametoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na fedha katika taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwasaidia baadhi ya wagonjwa waliopo katika hospitali hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufika katika Taasisi ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kutoa masaada wa vitu mbalimbali.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa na wafanyazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam.
......................................
Hata hivyo wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam wametoa elimu kwa wafanyakazi na wanakikundi cha 'The Great Ten'wa Kampuni ya Busines Times jijini Dar es Salaam kuhusiana na kufungua Akaunti ya MALKIA katika benki hiyo kwa kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo kilele cha maadhimisho ya siku hiyo ni Machi 8 kwa kila mwaka.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro (kulia) na Meneja wa huduma kwa mteja wa benki ya CRDB tawi la water Front jijini Dar es Salaam wakiwa katika kikao na wafanyakazi wa wafanyakazi wa kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten'.
Baadhi ya wafanyakazi wa wafanyakazi wa kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten'.wakimsikiliza Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro (kulia) na Meneja wa huduma kwa mteja wa benki ya CRDB tawi la water Front jijini Dar es Salaam leo.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...