Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .


VYOMBO vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu, raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini  Armenia.


Wanyama hao wakiwa kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia wanyama walikuwa wasafirishwe kwa ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa nchini Belarus kupitia kampuni ya Arusha Freight Limited ya jijini Arusha.


Raia hao wa Uholanzi waliokamatwa juzi majira ya saa 1:30 jioni katika uwanja wa ndege wa KIA wametambulika majina yao kuwa ni Arten Vardanian (52) aliyekuwa na hati ya kusafiria yenye namba NWF8CKJR8  na Edward Vardanian (46) aliyekuwa na hati ya kusafiria namba NY969P96.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa akiwa ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari.


Meneja usalama uwanja wa ndege KIA,Kisusi Justine aliliambia Tanzania Daima mbali na kukamatwa kwa raia hao wa kigeni pia walifanikiwa kumshikilia Mtanzania ,Idd Misanya anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.


“Wahusika hawa wawili walifika eneo la Cargo ambako walikuwa katika harakati za kusafirisha wanyama hao ndipo tulipowashikilia kwa sababu taratibu za kusafirisha wanyama Hai zilikiukwa”alisema Justine.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. WAZIRI MAGEMBE KAKULUPUKA TU HAKUNA CHA AJABU KATIKA HAO NYANI,HII NI BIASHARA HALALI NA HIVYO VIBALI NI HALALI,TANZANIA KILA MWAKA IMERUHUSIWA KUUZA VELVET MONKEYS 1600,NINACHOONA HAPA HATA WAANDISHI WA MAGAZETI WANASHABIKIA BILA KUDADISI KWANZA,MSIPOANGALIA SERIKALI ITALIPA PESA KIBAO HASARA YA KUZUIA NDEGE KUWEKA WATU NDANI WAKATI HAWANA MAKOSA,CHA MSINGI WAZIRI UNATAKIWA UWE NA UHAKIKA UNAPOTOA UAMUZI KAMA HUU AMBAO NI ASILIMIA MIA MOJA MAGEMBE KAKULUPUKA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiuungwana tu, mbona kama una hasira sana? Pia umejuaje mambo yote haya? Na ni kwa nini usimwachie waziri Magembe afanye kazi yake?

      Delete
    2. Pole sana Boss miaka hii 5 mnakazi! Heshima itakuwa mjini subiri zamu yako

      Delete
  2. Wewe anonymous wa kwanza nani kakwambia waziri kakurupuka. Hii serikali iko makini wanafanya kazi kwa uchunguzi kabla hawajakamata. Waholanzi hao hawana vibali na ndio maana wamekamatwa. Polisi sio wajinga wawaite waandishi wa habari kabla hawajahakikisha hao jamaa wametenda kosa. Pole ndugu mwaka huu mtanyooka mlizoea vya kunyonga sasa vya kuchinja vinawashinda. Acha waziri na serikali wafanye kazi

    ReplyDelete
  3. -WEWE WA NNE MCHANGIA MADA HUJUI,KITU.KWA KUWA TANZANIA INA QUOTA YA EXPORT YA VELVET MONKEYS 1600 KWA MWAKA,NA HAWA VELVET MONKEYS KILA MWAKA WANAUZWA NJE,HAKUNA CHA KUSEMA HII NI AWAMU NYINGINE LAKINI IFUATE SHERIA HATA UNAKURUPUKA TU ILI UONEKANE UNATUMBUA MAJIPU,HATWENDI HIVYO TARATIBU ZIFUATWE.NASEMA WAANDISHI WENGI WA MAGAZETI HAPA TANZANIA HAWAJUI KITU KUHUSU BIASHARA HII YA WANYAMAPORI.WANGEENDA PALE MPINGO HOUSE WAELEWESHWE TARATIBU SIYO KUANDIKA TU,HAO POLISI NDIYO HAWAJUI KITU KABISA WATAFANYA UCHUNGUZI GANI,SIKU YA MWISHO HAO WATAACHIWA TU BILA KOSA .MMEWAHARIBIA MUDA NDEGE IMESIMAMA BILA KUONDOKA NA MZIGO NK.MCHANGIAJI USISHABIKIE KITU AMBACHO HUJUI,MIMI NIPO KWENYE HII BIASHARA NAJUA KILA KITU NA TARATIBU UKWELI WAZIRI HUYU KAKURUPUKA NINA ASILIMA MIA NINACHOSEMA

    ReplyDelete
  4. Ndugu hakuna aliyebisha kwamba tanzania haifanyi biashara ya wanyama pori. Ila hili suala la waholanzinaalikuwa hawana vibali vya kusafitisha hao tumbuli. Na ndio maana sasa hivi wanafikishwa mahakamani. Umeshindwa kuelewa mchangiajia mada wa kwanza na wa tano ambayo i aonyesha ni mtu mmoja. Serikali hii iko makini ndugu hapa kazi tu, wewe endelea kutoa mapovu sisi tunajenga nchi ya wanyonge. Biashara unaijua weka jina lako sio unakuja kama anonymous halafu eti biashara unaijua!!!! Wacha usanii ndugu

    ReplyDelete
  5. Kuna watu humu ni kama mawakala wa wahalifu. Kawezi mawakili tu ili mtetee uchafu wote unaopita pale airport. Mimi binafsi nasapoti na ninamwamini JPM na jeshi lake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...