Wanafunzi waliomaliza kidato cha sita Shule ya Tambaza mwaka 1990 (Class of 99), leo wamekabidhi msaada wa vitabu vya sayansi shuleni hapo kama mchango wao kwa shule yao ya zamani
Akiongea na waandishi wa habari Mratibu wa Class of 99, Marsha Makatta Yambi amesema lengo ni kuhakikisha dhana ya Elimu bure inatekelezwa kwa kila mwenye kuguswa na matatizo ya Elimu kusaidia kwa kadri ya uwezo wake. Marsha amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto za maisha yao
Pichani Marsha makatta Yambi akimkabidhi makamu mkuu wa shule ya sekondari ya Tambaza vitabu hivyo ambavyo vimegharimu Shilingi Milioni Tatu na Laki Mbili.
Naye makamu wa mkuu wa shule ya Tambaza alishukuru kwa msaada huo ambao anasema ni wa kipekee na kuwaomba wanafunzi wengine waliohitimu shuleni hapo kuiga mfano huo sababu mahitaji ni mengi na serikali peke yake haitaweza kuyatimiliza bila ya msada wa wadau




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...