Kampuni ya simu ya Zantel leo imekabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye vifaa vya ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui Unguja vyenye thamani ya shilingi milioni 20. Vifaa hivyo ni mashine ya perkins brailler, index printer, braillon paper pamoja na salte na stylus.
Msaada huo umekabidhiwa na Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mohamed Mussa alisema vifaa hivyo ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya Zantel katika kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata elimu bora bila kujali tofauti zao.
‘Wajibu wetu kama wanajamii ni kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata msaada kama ilivyo kwa watu wengine na pia kuweza kuwaanda kwa ajili ya kuweza kufikia malengo yao kama walivyo kusudia’ alisema Mussa. Shule ya msingi Kisiwandui ilianzishwa mwaka 1991, na mpaka sasa wanafunzi 199 wamepitia shuleni hapo.
Mshauri
wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akizungumza wakati
akikabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule
ya msingi Kisiwandui. kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na
Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban.
Mshauri
wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akikabidhi vifaa vya
kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui
kwa Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid
Shaaban. Anayetazama katikati ni mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed. 
Mshauri
wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akizungumza wakati
akikabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule
ya msingi Kisiwandui. kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na
Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...