Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea na mikakati yake ya kusogeza huduma bora kwa wateja wake kwa kufungua duka lake la kwanza katika wilaya ya Kahama Mkoani, Shinyanga

Duka hilo la kisasa ni moja ya ahadi ya Airtel kujali wateja wake Tanzania nzima na kuwapa huduma iliyobora na ya kiwango cha juu popote pale walipo.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel, Adriana Lyamba alisema, “ Airtel imefanikiwa kuwafikia wateja kwa kufungua milango mjini Kahama na kuwahakikishia tunaendelea kuwa wabunifu kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora za kisasa zenye gharama nafuu kwa watumiaji wa simu za mkononi nchi

Duka hili ni la kwanza hapa mjini kahama, hivyo tunajisikia furaha sana kuleta huduma zetu karibu na wateja wetu na kuwapatia fursa ya kutumia huduma zetu kama vile Airtel Money kujiongezea kipato. 

Natoa wito kwa wakazi wa Kahama kupata nafasi ya kutembelea duka hili na kupata huduma pamoja na bidhaa mbalimbali ikiwemo modemu ya maajabu ya Airtel Wingle pamoja na simu orijino za smartphone kwa bei nafuu. Aliongeza Lyamba

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Vita Kawawa alisema “Kahama ni moja ya miji inayokuwa kwa kasi kubwa hivyo kufunguliwa kwa duka hilo kutaongeza ufanisi wa huduma za mitandano. 

Tunawashukuru sana Airtel kwa kuona ni vyema kutuletea huduma hii hapa mkoani na kutuhakikishia mawasiliano bora wakati wote na kuondoa changamoto zilizoko hapo awali. Kwa wakazi wa kahama huu ni wakati muafaka kutumia duka hili vyema ili kupata bidhaa zitakazotusaidia katika kuendesha shughuli zetu za uchumi na kijamii

Mpango huu wa Airtel kufungua maduka zaidi nchini, unalenga kuboresha maduka ya kampuni hiyo, ili yawe ya kisasa kama ilivyo katika mikoa ya mwanza, Arusha,Kilimanjaro na Mlimani City Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bwana Vita Kawawa akikata utepe wakati wa kuzindua duka jipya la kwanza na la kisasa la Airtel litakalowawezesha wakazi wa Kahama kupata huduma bora za mawasiliano, akishuhudia (kulia) ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel bi Adriana Lyamba , (kushoto) ni Meneja Mauzo wa Mkoa wa Shinyanga Bwana Ezekieli Nungwi.
Mfanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja Bwana Diliwish Tully akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bwana Vita Kawawa ( wa kwanza kushoto) juu ya vifaa na simu mbalimbali za smartphone zinazopatikana katika duka jipya la Airtel Kahama wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya na la kwanza wilayani hapo. Akishuhudia (katikati) Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel bi Adriana Lyamba.
Wakazi wa wilaya ya kahama wakiangalia simu ya smartphone ya Bravo Z 10 inayopatikana katika duka jipya la Airtel Kahama wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya na la kwanza wilayani hapo litakalowawezesha wakazi hao kupata huduma bora za mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...