Na Woinde Shizza,Arusha 

MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za kiganjani zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha desemba hadi February mwaka huu ziko salama na sio za bandia ,huku asilimia 18 zikionekana zikiwa za bandia hivyo kuwataka wananchi kutambua kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache tofauti na kipindi cha nyuma. 

Pia imebainika kuwa asilimia kubwa ya nyumba zinazoungua na umeme ni
kutokana na simu bandia ambazo betri zake au vifaa vyake hushindwa kuhimili 
mionzi pindi zinapokuwa zinachajiwa hivyo kusababisha mlipuko wa moto na 
hivyo kuleta madhara . 

Hayo yalisemwa na meneja uhusiano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania
Innocent Mungi alipokuwa akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya 
namba za utambulisho wa simu za kiganjani iliyowashirikisha wadau na
wafanyabiashara wa jijini hapa. 

Alisema kuwa kutokana na elimu ambayo wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu 
hizo ya kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi imepunguza uingizaji 
wa simu feki na kwamba wamebaini kuwa asilimia 79 ni salama hazina matatizo 
ya aina yeyote. 

Alidai kuwa kufuatia uzimaji wa simu bandia litakalofanyika juni 16 mamlaka
hiyo imeweza kutoa elimu kwa wauzaji,watumiaji ili kuhakikisha kuwa 
wanabini simu zao kama ni salama ili kuweza kuepuka zoezi la kuzimiwa simu 
zao bila yawao kujiandaa. 

“wakati tumeanza kubaini zoezi la kutambua simu feki tulibaini kuwa
asilimia 30 zilikuwa bandia ila kutokana na elimu iliyotolewa hadi February
simu bandia zimepungua hadi kufikia asilimia 18 hii inaonyesha kuwa simu
feki zilizoko sokoni ni chache mno “aliongeza .

Aidha Innocent alitaja faida za kuzimiwa simu bandia kuwa ni pamoja na
kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu ,kupunguza wizi wa simu 
na kupunguza matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitumika mara nyingi kwa 
njia ya simu hizo pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango. 

Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Ally Simba aliwataka wananchi
kufanya zoezi la kuhakiki simu zao kwa kufuata maelekezo sahii ili waweze
kubaini simu feki kabla ya kuzimiwa simu hizo juni 16 ,kwani wengi wa
watumiaji wa simu hawafuati malekezo ya kutambua simu bandia . 

Simba aliseama kuwa ni vema wananchi wakatumia mfumo waliowekewa wa kubaini 
simu zao kama ziko salama kwani ifikapo juni simu zote bandia zitazimwa na 
kuwataka wafanyabiashara nao wawe makini pindi wanaponunua mizigo yao ya 
bashara ili kuepuka hasara watakazozipata wao na pia hasara watakazopata 
wanunuzi wa simu hizo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...