Mhandisi wa Baraza la Manispaa Mzee Juma Khamis wa kwanza kutoka kulia akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyefanya ziara kuangalia baadhi ya Mitaro iliyosababisha mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Nd. Said Juma Ahmada.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili a Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Abdoud Mohammed akimueleza Balozi Seif hatua zilizokwisha chukuliwa na watendaji wa Kamati ya Maafa katika kunusuru maafa yaliyojitokeza ndani ya kipindi cha mvua zilizoleta athari kubwa.
Balozi Seif akiwafariji Baadhi ya Wananchi wa Mitaa ya Kwahani, Kwawazee na Sebleni ambao nyumba zao zimeathirika kwa mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia Jumapili.
Skuli ya Nyerere Sekondari ni miongoni mwa skuli zinazotoa huduma ya muda ya kuwahifadhi watu walioathirika na mvua kubwa za juzi ambapo Balozi Seif alipata wasaa wa kuwatembelea kwa kuwapa pole.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...