Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Chabaka Kilimunga alikutana na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Comoro (TADICO), tarehe 27 Aprili 2016 katika ofisi za Ubalozi jijini Moroni.

Pamoja na mambo mengine, uongozi huo mpya wa TADICO uliwasilisha katika yake mpya na kueleza mikakati iliyonayo ya kuboresha utekelezaji wa shughuli za TADICO kwa manufaa ya wanadiaspora waishio Comoro.

Aidha kwa upande wake Mh. Chabaka alieleza kufurajika na uongozi huo mpya kuja kumtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha ambapo aliuambia uongozi huo kuwa, Serikali inatilia mkazo mkubwa sana wa ushiriki wa wanadiaspora katika maendeleo ya nchi wanazotoka, hivyo ni muhimu kwa uongozi huo kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuchangamkia fursa mbalimbali zinazoibuka kutoka nyumbani.

Sambamba na hilo Mhe. Chabaka aliendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya Ubalozi na uongozi wa TADICO.
Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Comoro (TADICO), mara baada ya kukutana nao kwa mazungumzo. Kutoka kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ahmed Mzee Mbaba, Mweka Hazina wa Jumuiya, Suzan Harun Kalambo, Afisa Ubalozi, Thabit A. Khamis, Mkuu wa Kanseli Ubalozi, Mudrick Soragha, Mwenyekiti wa Jumuiya, Omari Kombo Hussein pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Frank John Kalambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Big up mhe. Balozi Chabaka na uongozi wote kwa jumla. mkuu wa kanseli Ndugu Soragha mtu poa sana tena sana hana majungu ubalozi utakuwa na amani. bwana afisa wa ubalozi Ndugu Thabiti nae poa sana yupo juu juu zaidi.
    Hongereni wote hiyo timu imetulia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...