Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mchana huu ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna Kilango Malecella, kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa wakati kumbe wapo wengi tu.

Rais Magufuli amesema kwamba hakuamini kwamba kuna mkoa ambao hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuweko na wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanya.

Rais Magufuli, ambaye alikuwa anaongea baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU  toka kwa Mkurugenzi wake Mkuu  Valentino Mlowola,  amesema kasikitishwa sana na kauli ya Mama Malecela ambaye bila shaka alikuwa amepata ushauri mbaya toka kwa watendaji wake. 

Amesema idadi hiyo ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili zilikuwa bado zinaendela kuhakikiwa.
Rais Magufuli amesema pia kwamba hadi jana jumla ya wafanyakazi hewa zaidi ya 5, 507 wamebainika nchi nzima, wengi wao wakitoka katika halmashauri.

Hivyo Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi. Wakuu wa mikoa waliapishwa mwezi uliopita.

Katika siku hiyo Rais aliwapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika Orodha ya Malipo ya Mshahara (Pay Roll) wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini, na kuwataka wakuu wa Mikoa hao wasimamie zoezi hilo kwa ukamilifu. 

Vile vile Rais Magufuli alionya kuwa halmashauri yoyote baada ya muda huo itakayokuwa na mfanyakazi hewa, mkurugenzi wake atakuwa amejifuta kazi mwenyewe.Vilevile Rais amewaagiza mawaziri wote kuwaeleza watendaji wao wawaondoe wafanyakazi hewa wote ndani ya kipindi hicho cha siku 15 na kubainisha kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watafukuzwa kazi kwani sheria ni msumeno.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Inasikitisha kufukuzwa kazi hata ndani ya muda mfupi kw ajili ya kutokuwa mkweli( dishonesty ). Hii pia iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo. Ikumbukwe kuwa suala la kusema ukweli kwenye hili zoezi lilisisitizwa sana na Mh. Rais kuwa wakawe waadilifu na wafanye kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  2. Pole mama. Labda ulisahau kuwa katika serikali hii hakuna siasa na maneno matamu ya kupambana na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa. Enzi za kufanyakazi kisiasa zime kwisha. Wafanyakazi na watendaji badilikeni. Mbona Kenya wanafanyakazi kwelikweli na wanapiga hatua?

    ReplyDelete
  3. Kweli sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma na haijali ni type gani ya mbao.

    ReplyDelete
  4. The mdudu, huyu mama anacheza na maisha ya watanzania mimi kwajinsi nnavyo wapenda akina mama na dada zangu lakini kwa ujinga na uzembe huu utanisamehe mama na zawadi yangu kubwa kwako ni KARIBU kwenye maisha duni kama yangu hii ndio ilikua mizigo isio bebeka kipindi cha Kikwete Asante sana rais wetu mpendwa na makini JPM pamoja sana

    ReplyDelete
  5. Sasa nimeamini aliposema hapa kazi tu alimaanisha. Mungu akulinde mh rais wetu

    ReplyDelete
  6. Ndo maana neno 'kuula' halisikiki tena, hapa kazi tu

    ReplyDelete
  7. Honest is number one criteria for keeping your job in the West.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siku zote uaminifu ni mtaji, I'm with on that one

      Delete
  8. MIMI SIYO MWANDISHI MZURI WA KWENYE BLOGS....LAKINI KWA HILI LAZIMA NIANDIKE TENA KWA CAPITAL LETTERS. RAIS MAGUFULI NAKUPA PONGEZI KWA HILI, UMEONYESHA KUWA SHERIA NI MSUMENO UNAKATA SEHEMU ZOTE MBILI HAUCHAGUI NANI NI NANI....AHSANTE RAIS KWA KUTETEA MAISHA YA WATANZANIA, ANGALAU WATANZANIA WATAPATA DAWA NA HUDUMA BORA HOSPITALINI KWA KUWA PESA NYINGI ZILIZOIBIWA NA WASIO WAAMINIFU ZITARUDI KWENYE MFUMO NA KUSAIDIA MASHULE ILI WATOTO WETU WASIENDELEE KUKAA CHINI NA NDUGU ZETU NA SISI TUSIFE KWA KUKOSA MADAWA KWENYE MAHOSPITALI ZETU. WANAOIBA WANAFANYA MAISHA YAWE MAGUMU......WAPEWE ADHABU KALI NA WAFILISIWE. TUIPENDE NCHI YETU NA WATU WAKE....TUWAONDOE HAO WEZI WANAOFANYA NCHI IWE MBAYA.

    ReplyDelete
  9. Miye simtetei mtu wala kumpinga mtu, ila nataka kusema kwamba huyu
    mama kazi alipewa majuzi tu, na huo wizi bila shaka ulikuwa upo hapo miaka kadha iliyopita. Je huwezi kufikiri kwamba yeye huyo mama ni victim wa wizi pia na kosa lake ni kutowatambua majizi waliomzunguka.Everybody deserves a second chance.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Awamu zilizopita hata 10th chance ungepata, hizi ni zama za hapa kazi tu bana

      Delete
  10. Tanzania kwa mara ya pili imepata raisi baada ya Nyerere

    ReplyDelete
  11. Second chance and third chance was last gavament ...this one hapa kazi tuu ...will take long time but hopefully tutafika.....god bless our president. .

    ReplyDelete
  12. Wewe unayemtetea huyu aliyefukuzwa hufikirii vizuri. Wakuu wa mikoa walipewa muda kufichua matumishi hewa. Hata kwa akili ndogo tu kwa uzembe wa huko nyuma haiyumkini kuwa na mkoa usiokuwa na mtumishi hewa. Kama yeye mkuu wa mkoa alipewa taarifa za uongo na wasaidizi wake, alichukua hatua gani kujiridhisha? Kama Rais amefikia kutuma tume ya uchunguzi mkoani kwake, kwa nini yeye mkuu wa mkoa hakufuatilia? Na tume aliyoituma Rais inakaa hotelini na inalipwa allowance, hizi fedha ni hasara kutokana na uzembe wa mkuu wa mkoa. Kama huyu mkuu wa mkoa aliamua kufisha huu ufisadi au kukosa judgement au kudharau na kutotoa uzito kwa hatua zinazochukuliwa sasa na rais mpenda Magufuli, basi huyu hatufai. Ni jipu na atupishe. Watu kama hawa wakibaki ndOi wanakuja kuupa upinzani mambo ya kusema! Chini ya utawala wa mMagufuli upinzani utakufa natural death. Kama huamini mwambie Magufuli azunguke mikoani sasa uone atakavyovuna kadi za wapinzani!

    ReplyDelete
  13. Kwanini awe ana-deserve second chance wakati walipewa muongozo na kuambiwa nini cha kufanya. Halafu yeye bila kufanya utafiti wa kutosha anakwenda kusema uongo.....Kumbuka makosa hayo yanasababisha serikali inaibiwa bila huruma na wezi wanaachwa tu na viongozi wanaruhusu tu wizi uendelee. waondolewe na wasifanye kazi kabisa tena serikalini.

    ReplyDelete
  14. Licha ya kazi ya miaka mingi ya kuonyesha utovu wa kuwepo na wafanyakazi hewa - kazi aliyofanya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali na mashirika yake, yako madudu na viwavi wa mbu na mainzi yenye kuzidisha kuzalisha mbu na mainzi zaidi katika ununuzi wa vifaa na huduma kutoka kwa kampuni za jamaa zao na marafki au kushirikiana na matajiri wezi katika kupandisha bei za vifaa na huduma kumbe vifaa na huduma zifikazo maofisini ni uduchu kweli!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...