Mwimbaji nyota wa Mashujaa Band Chaz Baba, leo usiku atakwea jukwaa la Mashauzi Classic ndani ya Mango Garden Kinondoni katika onyesho maalum la “Usiku wa Kismet”.

Katika onyesho hilo, Chaz Baba ataimba wimbo wa Isha Mashauzi “Nani Kama Mama” pamoja na vionjo vyake kadhaa vya nyimbo zake za dansi.

Usiku wa Kismet umeandaliwa maalum kwaajili ya watu kujiachia na wapenzi wao ambapo pia CD za wimbo wa “Kismet” zitatolewa kama zawadi ukumbini.

“Kismet” ni wimbo mpya wa Mashauzi Classic ulioimbwa na Isha Mashauzi ambao umejaa maishairi matamu ya mapenzi.

Akiongea na mtandao huu, Isha Mashauzi ambaye ndiye bosi wa Mashauzi Classic, alisema mashabiki watakaoweza kuimba kwa ufasaha japo mstari mmoja wa wimbo “Kismet” watazawadiwa zawadi ya fulana za Mashauzi Classic.

Awali “Usiku wa Kismet” ulikuwa ufanyike Alhamisi iliyopita lakini ukaahirishwa kutokana na mvua mkubwa iliyonyesha katika muda mwingi wa onyesho hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...