Paschal Lugali, mfanyakazi katika Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu akipanga miche ya miti ya matunda mapema leo, ikiwa ni ahadi ya
serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira
Afisa Misitu Mwandamizi kutoka Idara ya Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Raisi bw. George Kafumu akiangalia miche ya miti ya matunda
baada ya kuiwasilisha katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mapema Leo.
Miche ya miti ya matunda, ikiwa imepangwa baada ya
kupokelewa mapema Leo katika halmashauribya wilaya ya Meatu,baada ya serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira kutekeleza ahadi yake ya
kugawa miti elfu ishirini na saba (27,000) Katika mkoa wa Simiyu.
Baadhi ya wakazi wa jimbo
la kisesa mkoani Simiyu katika picha pamoja na miche ya miti ya matunda waliyo
ipokea kutoka serikalini kupitia Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakishusha
miti ya Matunda kutoka kwenye gari iliyoibeba mapema leo, miti hiyo waliahidiwa
na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Makamu wa Raisi)







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...