Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiwa ameongozana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan (kuahoto) mara baada ya kumpokea katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam. Mhe. Zhang Jiannan pamoja na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi kwenye Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na kuimarisha ushirikiano baina ya Mahakama ya Tanzania na China.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China uliolenga kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa Mahakama za Tanzania na China leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China.
Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wale wa Mahakam Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakibadilisha uzoefu wa shughuli za kimahakama na masuala mbalimbali ya utendaji wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China jijini Dar es salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...