Mkurugenzi Mkuu wa Maxmalipo  Juma Rajabu akifafanua jambo kwa wakurungezi wa serikali za mitaa kutoka Uganda , Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji Kanda Group COO – Maxcom Africa Jamson Kassati , Kushoto Mwanzo Mr. Moses Kimaro Kutoka ALAT (jumuiya ya serikali za MItaa Tanzania)  na pembeni yake katikati ni Mwenyekiti wa wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka Uganda Dunstan Balaba ambapo Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara Kutoka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari Akifafanua Jambo kwa Wakurugenzi hawa kutoka Uganda, Akielezea Jinsi mfumo wa Ukusanyaji Kodi na tozo mbalimbali ulivyorahisisha upatikanaji wa mapato katika halmashauri mbalimbali na Taasisi za Serikali kwa Ujumla na kuzuia mianya ya upoteaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali vya halmashauri.
Mwenyekiti  na Msemaji wa Umoja wa wakurugenzi kutoka Uganda  Bwana Dunstan Balaba Akieleza Jambo kwa Hadhara na Kukiri kushangazwa na watanzania Kuweza Kugundua Teknolojia kama hii. Pia Kumwomba Mkurugenzi wa Maxmalipo Afungue Ofisi Uganda Mapema iwezekanavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...