Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe akisisitiza jambo mbele ya vijana wa Kitanzania waishio New York, Marekani, jana. Mhe Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana hao waliotaka kujua maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya bunge la jamhuri anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi kupitia upinzani, pia yeye kama mwana siasa alie upande wa upinzani nini mtazamo wake juu ya kasi ya Rais wa wamu ya 5. Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University New York na kuongea na wasomi wa huko na pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard University huko Boston. MA. Picha na Vijimambo Blog New York
Zitto akipata ukodak baada ya kukutana na Watanzania New York City. Kwa taswira zaidi nenda soma zaidi.
Zitto akitafakari swali kabla kujibu, Zitto aliulizwa kama yupo tayari kuungana na Ukawa na kama yupo tayari kungombea kiti cha urais kupitia chama chake ACT, majibu yalikuwa yupo tayari kuungana na UKAWA lakini anaitaji kujua nini faida ya kuungana na kama kuungana ili kuing'oa CCM basi iwe na nguvu kweli kweli na ifanikiwe kwani asingependa kuungana na na kubakia msindikizaji tu bila faida endelevu na kama yupo tayari kugombea kiti cha urais basi atafanya hivyo akiwa amesha jiandaa vilivyo ili akigombea apate ushindi wa kishimdo na kuing'oa CCM na siyo vinginevyo.
Hapa ni Patel akiuliza swali kwa Zitto, Patel ni Mtanzania mwenye asili ya India ndiyo aliandaa mkutano huu kwa kushirikiana na Nasaan Chiume.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...