Na Bashir Yakub.
Ni ukweli usiofichika kuwa kisheria deni linafunga. Hii ni tofauti na wengi wanavyoamini. Wako watu hukopeshwa hela na hukaidi kulipa au kulipa bila kuzingatia makubaliano kwa kuamini kuwa mdai wake hatakuwa na la kufanya kwakuwa deni halifungi.
Na hii mara nyingi huwatokea wale ambao wametoa mikopo bila hata rehani yoyote.
Mkopo kwa rehani huwa haumsumbui mtoa mkopo kwakuwa mrejeshaji anapokaidi rehani huchukuliwa. Lakini pasipo na rehani huwa inahitajika nguvu za ziada kumfanya mdeni alipe.
Ni vema kuliweka sawa hili la deni kufunga ili wale waliodhulumiwa haki zao wachukue hatua na wale wenye mpango wa kudhulumu kwa mgongo wa deni halifungi waache au wadhulumu lakini wakijua kuwa hatua dhidi yao zaweza kuchukuliwa.
1.KUFUNGWA.
Moja ya tofauti inayojulikana sana kati ya kesi za jinai na mashauri ya madai ni hii kuwa kesi za jinai mtu atakamatwa atazuiliwa na pengine baadae akionekana ana hatia adhabu yake itakuwa kufungwa. Hii ni tofauti na zile za madai ambapo hamna kukamatwa wala kuzuiliwa na hukumu zake hazihusu kufunga.
Kwa ujumla(general rule) kesi za madai hazifungi isipokuwa yapo mazingira ambapo zinaweza kufunga. Moja ya mazingira hayo ni pale ukaidi wa kutolipa deni unapojitokeza. Tutaona zaidi kuhusu hili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...