Msanii wa bongo fleva Saraha ambaye ni raia wa Sweden ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden jijini Stockholm leo na kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi Dora Msechu.
Saraha hivi sasa anatamba kwenye anga za muziki nchini Sweden na nyimbo ya "Kizunguzungu" ambayo ameimba kwa lugha ya kiswahili.
Balozi Dora Msechu amempongeza Saraha kwa mafanikio makubwa aliyopata kwa wimbo huo ikiwa ni pamoja na kuingia fainali ya mashindano makubwa ya kutafuta nyimbo bora hapa Sweden, Melodifestivalen.
Mhe. Balozi amemshukuru sana Saraha kwa kuitangaza vyema Tanzania na kusambaza lugha ya kiswahili nchini Sweden kupitia fani ya muziki.
Kwa upande wake, Saraha ameeleza kuwa amepata faraja kubwa sana kukaribishwa na Mhe. Balozi kutembelea Ubalozi wa Tanzania na amefurahi sana kupata fursa ya kuzungumza Kiswahili.
Saraha amesema kuwa ana mapenzi makubwa sana na Tanzania na ataendelea kutumia lugha ya kiswahili katika kazi zake za usanii hapa Sweden. Amebainisha kuwa hivi sasa yupo mbioni kutoa nyimbo nyingine kali ya kiswahili hapa Sweden.
Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu akiongea na mwanamuziki Saraha na meneja wake walipotembelea ubalozini jijini Stockholm leo.
Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu akipozi na mwanamuziki Saraha alipotembelea ubalozini jijini Stockholm
Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu na watumishi wa ubalozi wakipozi na mwanamuziki Saraha alipotembelea ubalozini jijini Stockholm. Cheki video yake ya ngoma yake kali ya "Kizunguzungu" hapa chini.
Huyu ni dada yake mzunvu kichaa? Naona atamshinda Diamond kabisa. Nice song!
ReplyDelete