Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kikazi Gereza Kwamugumi, Korogwe Mkoani Tanga, kesho Aprili, 15 2016.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja inaeleza kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea maendeleo ya mradi wa mabwawa ya samaki yaliyopo gerezani hapo ambayo hadi sasa yamepandwa vifaranga wa samaki 18,800 tangu tarehe 16/12/2015.

Kabla ya kutembelea eneo la mradi wa mabwawa ya samaki, Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha atapokea taarifa fupi ya maendeleo ya mradi wa uzalishaji samaki Gereza Kwamugumi, Korogwe.

Miradi ya ufugaji samaki ipo katika Magereza ya Karanga, Njombe, Masasi, Tukuyu ambapo nia ya Uongozi wa Jeshi la Magereza ni kuieneza katika Magereza mbalimbali yenye fursa za kuendesha mradi huo.

Mradi wa uzalishaji samaki katika Gereza Kwamugumi ni mojawapo ya miradi mbalimbali ya uzalishaji mali iliyoanzishwa na Uongozi wa Jeshi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi la Magereza, hususan katika kuipunguzia Serikali gharama za kuhudumia Magereza na kuongeza pato la kodi kwa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...