Uongozi wa
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kuongezwa kwa safari moja ya ziada
kwa kila awamu ya usafiri huo kuanzia siku ya Jumatatu Aprili 25, 2016. Hivyo
basi awamu ya asubuhi na ile ya jioni itakuwa na safari 4 badala ya 3 za sasa,
halikadhalika muda wa kuanza safari nao umebadilishwa.
Kwa awamu
ya asubuhi treni ya kwanza itaondoka Ubungo Maziwa kuja kituo kikuu cha Dar es Salaam
saa 12:15 ambapo itawasili saa 12:55. Safari ya mwisho ya nne itaondoka Ubungo
Maziwa saa 5:15 asubuhi kwenda Kituo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kwa awamu
ya jioni kutoka Kituo Kikuu cha treni cha Dar es Salaam safari ya kwanza
itaanza saa 10:00 jioni itawasili Ubungo
Maziwa saa 10:40 jioni. Safari ya pili kutoka Kituo cha Dar es Salaam itaanza
saa 11:40 na kuwasili Ubungo Maziwa saa
12:20 jioni. Halikadhalika safari ya 3 itaanza kutoka kituo cha Dar es Salaam
saa 01:20 usiku na ile ya 4 saa 3:00 usiku kwenda Ubungo Maziwa.
Halikadhalika
taarifa hii ya mabadiliko ya safari za treni ya jiji imeainisha kuwa Kituo cha
Kamata kitatumika kwa safari zote 4 za awamu ya jioni kwenda Ubungo Maziwa na kurudi Kituo cha Dar es Salaam.
Uamuzi huu
umechukuliwa ili kukidhi maombi ya abiria waliokuwa wanataka kituo cha Kamata
kitumike kwa huduma ya treni ya Jiji awamu ya jioni.
Aidha wito
maalum umetolewa na Uongozi wa TRL kuwa abiria na wadau wote wa huduma ya treni
ya Jiji kufuata kwa makini maelekezo ya wahudumu wa treni hiyo ili kuongezwa
kwa safari za huduma hiyo kuwe na tija kwa abiria na Kampuni ya TRL.
RATIBA MPYA YA TRENI YA JIJI KUANZIA APRILI 25, 2016
AWAMU YA ASUBUHI
|
KITUO
|
KUWASILI
|
KUONDOKA
|
|
|
UBUNGO MAZIWA
|
SAA 12:05
|
SAA 12:15
|
|
|
DAR
|
SAA `12:55
|
SAA 01:05
|
|
|
UBUNGO MAZIWA
|
SAA 01:45
|
SAA 01:55
|
|
|
DAR
|
SAA 02:35
|
SAA 02:45
|
|
|
UBUNGO MAZIWA
|
SAA 03:25
|
SAA 03:35
|
|
|
DAR
|
SAA 04:15
|
SAA 04:25
|
|
|
UBUNGO MAZIWA
|
SAA 05:05
|
SAA 05:15
|
|
|
DAR
|
SAA 05:55
|
|
|
AWAMU YA JIONI
|
|
|
|
|
|
DAR
|
|
SAA 10:00
|
|
|
UBUNGO MAZIWA
|
SAA 10:40
|
SAA 10:50
|
|
|
DAR
|
SAA 11: 30
|
SAA 11:40
|
|
|
UBUNGO MAZIWA
|
SAA 12:20
|
SAA 12:30
|
|
|
DAR
|
SAA 01:10
|
SAA 01:20
|
|
|
UBUNGO MAZIWA
|
SAA 02:00
|
SAA 02:10
|
|
|
DAR
|
SAA 02:50
|
SAA 03:00
|
|
|
UBUNGO MAZIWA
|
SAA 03:40
|
SAA 03:50
|
|
|
DAR
|
SAA 04:30
|
|
|
Imetolewa
na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Masanja
Kungu Kadogosa
Dar es
Salaam,
Aprili 22,
2016.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...