Mwathirika ambaye pia ni mwenye matatizo ya goti tangu vita vya Kagera, Matern Ndimbo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
WAATHIRIKA wa vita vya Kagera vilivyoanza mwaka1978 hadi 1979 kati ya Tanzania na Uganda wameiomba serikali kuwakumbuka kwani walipata ulemavu walipokuwa vitani.
Hayo yamesemwa na mwathirika wa vita vya Kagera, Matern Ndimbo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa walioathirika katika vita vya Kagera ambao bado wapo hai mpaka sasa wanaomba kukumbukwa na serikali ya awamu ya Tano.
Ndimbo ameiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la pekee kwani ndio waliopigana vita vya Kagera ambavyo vilikuwa kati ya Tanzania na Uganda na kupata ulemavu.
Amesema kuwa kupata ulemabu isiwe sababu ya kuishi maisha ya kuhangaika kwani kipindi cha vita walikuwa msaada mkubwa kwa nchi.
Pia ameiomba serikali kwa siku ile ya Julai 25 ya kila mwaka ambapo huadhimishwa siku ya mashujaa ameomba serikali iwakumbuke kwa kuwajengea nyumba za kuisha na familia zao kwani kwa uongozi wa awamu ya tano unaweza kuwa msaada kwao.
"Mashujaa hai ndio wa kumbukwa sana kwani bado tunaweza kusimulia ilikuwaje, ikiwa na mashujaa waliofariki ni mhimu kuwakumbuka nao kwakuwa walipigania nchi yetu". Amesema Ndimbo.
Ni sawa kabisa ni muhimu wasaidiwe ikiwa ni shukrani maana hawa watu walitusaidia sana wananchi kagera.Hali ilikuwa mbaya.Wanastahili pongezi na misaada kuboresha maisha yao kwa kazi nzuri waliyofanya.Asante sana Mzee Ndimbo na mashujaa wenzako.
ReplyDelete