SIMU.tv: Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, yatangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria watoa huduma wa mawasiliano watakaoshindwa kulipia madeni wanayodaiwa. https://youtu.be/XWolro6NAZg
SIMU.tv: Mamlaka ya mapato nchini TRA kwa kushirikiana na jeshi la polisi wafanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali za matumizi ya binadamu zilizokuwa zikiingizwa nchini kwa njia zisizo halali kupitia bandari bubu. https://youtu.be/ZkfWp2WZnWk
SIMU.tv: Halmashauri ya wilaya ya Mtwara vijijini kwa mara ya kwanza yapokea milioni 150 kutoka shirika la maendeleo ya petrol nchini TPDC , ikiwa ni tozo ya uchakataji na usafirishaji wa gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. https://youtu.be/PnqdNHr8GwI
SIMU.tv: Ujenzi wa daraja la Buguruni uliokwama kwa zaidi ya miezi 8 hatimaye waanza hii leo baada ya mkandarasi mpya kupatikana na kuanza kazi.https://youtu.be/Vew3XEub3hU
SIMU.tv: Wanafunzi wa shule ya msingi Ipuli iliyoko manispaa ya Tabora wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kufuatia mvua zinazonyesha zilizopelekea kutuama kwa maji. https://youtu.be/RFvt3HiUOgQ
SIMU.tv: Wananchi wa Zanzibar waadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa nchi hiyo hayati Abeid Aman Karume na kutaka aenziwe.https://youtu.be/dSyGTlxpRsg
SIMU.tv: Rais John Magufuli na Mkewe bi Janeth Magufuli waungana na wananchi wa Rwanda kuadhimisha miaka 22 ya mauaji ya kimbari yaliyoua watu milioni 1.https://youtu.be/473D0Sav5ik
SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera amsiamamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya Hanang kufuatia tuhuma za ubadhilifu.https://youtu.be/YN1_MxnUa2s
SIMU.tv: Serikali yasema inakusudia kuzifanya hospitali zote za rufaa nchini kuwa chini ya wizara ya afya kutoka TAMISEMI. https://youtu.be/jc4hvDY81QE
SIMU.tv: Mkutano mkuu wa jumuiya za serikali za mitaa nchini ALAT, wamchagua Gullam Hafeez kuwa mwenyekiti wake mpya kwa kipindi cha miaka 5.https://youtu.be/NNJpsmZmeE4
SIMU.tv: Shirika la umeme nchini mkoa wa Ilala latoa sababu za kukosekana kwa umeme kwa siku kadhaa huku likidai kuwa ni matokeo ya uchakavu wa miundombinu.https://youtu.be/1Em_yHnk43Y
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...