Na John Nditi, Morogoro

MWENGE wa Uhuru umemaliza mbio zake mkoani Morogoro na umekabidhiwa mkoa wa Tanga mnamo Aprili 25 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na mbio zake katika muda wa siku kumi kwenye Halmashauri 11 zilizomo mkoani humo, imeelezwa.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kabwe aliukabidhi Mwenge wa Uhuru na wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mkuu wa mkoa mwezake wa Tanga, Martine Shigela , katika Kijiji cha Kikunde,kilichopo wilayani Kilindi .

Kijiji cha Kikunde kilichopo katika wilaya hiyo kinapakana na kijiji cha Iyogwe kilichopo wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro.

Kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa mkoa mwezake huyo, Dk Kebwe alisema , Mwenge wa Uhuru ulipokuwa mkoani Morogoro ulipitia miradi 41 yenye thamani ya Sh bilioni 9.4 ikiwa ni ya kuonwa , kuwekewa mawe ya msingi na kuzunduliwa.

Mwenge wa Uhuru ulizinduliwa katika mkoa wa Morogoro , Aprili 18, mwaka huu na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan , katika uwanja wa Jamhuri wa mjini Morogoro na kukimbizwa kwenye halmashauri saba kati ya nane zilizopo mkoani humo.

Kauli mbiu za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu (2016): “ Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa , Washirikishwe na Kuwezeshwa “.

Naye Mkuu wa mkoa wa Tanga, Shigela,alisema Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani humo utapitia miradi 78 yenye dhamani ya Sh bilioni 22.7 na utakimbizwa kwa muda wa siku 10 katika halmashauri 11 zilizomo mkoani humo na mara baada ya kukabidhiwa ulianza mbio zake katika wilaya ya Kilindi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe (kushoto) akitoa taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru wakati wa kumkabidhi Mwezake wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela.
Wakuu wa mikoa , Morogoro pamoja na Tanga wakikabidhiana Mwenge wa Uhuru mpakani mwa mikoa hiyo , Aprili 25, mwaka huu.
Furaha ya wauguzi na madaktari wa Kituo cha Afya Gairo , wakati Mwenge wa Uhuru ulipozindua jengo la wodi ya wanaume , Aprili 24, mwaka huu (mwenye kushika karatasi ) ni Mkuu wa wilaya ya Gairo, Khanifa Karamagi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...