Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hivi karibuni iliupongeza Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) kwa kazi nzuri ya kudhibiti madini yanayotoroshwa nje ya nchini
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala huo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016, walisema kuwa wakala umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mapato katika sekta ya madini na kuitaka serikali kuuwezesha zaidi ili uweze kuzalisha zaidi na hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kupitia sekta ya madini.
Mjumbe wa kamati hiyo, Suzan Kiwanga alisema kuwa TMAA ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi ya kudhibiti madini yanayotoroshwa nje ya nchi kupitia wataalam wake walioko migodini na viwanja vya ndege, hivyo ni vyema wakawezeshwa ili kufanya kazi hiyo kwa bidii na uaminifu mkubwa.
“Kulingana na ripoti yao, TMAA imefanya kazi kubwa ya kuokoa mabilioni ya shilingi kupitia ukamataji wa madini yaliyokuwa yanatoroshwa nje ya nchi, kazi waliyoifanya ni kubwa yenye kuhitaji uaminifu mkubwa, hivyo wakiwezeshwa zaidi wana uwezo wa kufanya vizuri zaidi,” alisema Kiwanga
Naye mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Ikupa Alex aliongeza kuwa wahalifu wanaokamatwa na TMAA wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria na kutozwa faini kubwa ili iwe fundisho wa watoroshaji wengine.
“ Huu wakala ndio unaowezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kubaini kodi inayostahili kulipwa na makampuni yanayojishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa madini nchini, rai yangu ni wakala huu kuwezeshwa zaidi katika nyanja zote ikiwamo rasilimali fedha na rasilimali watu ili uweze kufanya kwa ufanisi zaidi,” alisema Alex.
Awali akielezea mafanikio ya TMAA tangu kuanzishwa kwake Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Dominic Rwekaza alisema kwa kipindi cha mwaka 2009 hadi Januari 2016, kampuni mbalimbali zimelipa jumla ya Shilingi bilioni 680.5 kama kodi ya mapato.
Alifafanua kampuni hizo kuwa ni pamoja na Geita Gold Mining Limited iliyolipa jumla ya Shilingi bilioni 502.7 tangu kampuni hiyo ilipoanza kulipa kodi ya mapato mwaka 2009; Resolute Tanzania Limited iliyolipa kodi ya mapato kiasi cha Shilingi bilioni 100.4 katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 na Mgodi wa Dhahabu wa Tulawaka uliolipa Shilingi bilioni 77.4 kama kodi ya mapato mwaka 2012.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Dominic Rwekaza (pichani) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala huo kwa mwaka wa fedha 2015/2015 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Dominic Rwekaza (mbele) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala huo kwa mwaka wa fedha 2015/2015 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini.

Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini taarifa utekelezaji wa majukumu ya Chuo cha Madini Dodoma (MRI) kwa mwaka wa fedha 2015/2016, iliyokuwa inawasilishwa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Musa Magufuli (hayupo pichani).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...