Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, linapenda kutoa taarifa sahihi juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu TPDC kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic.

Ni vyema ikaeleweka kwamba, Akaunti ya  ESCROW  ni Akaunti  maalumu inayoweza kufunguliwa  baina ya  Kampuni, Taasisi,  au Mashirika mbalimbali ya binafsi na yale ya umma kwa matumizi maalumu. Lengo la Akaunti ya ESCROW ni kuhifadhi fedha au kupitisha malipo kwa ajili ya shughuli maalum ikiwemo miradi au kazi yoyote maalumu na malipo haya hufanyika baada ya pande mbili kuridhia. 

TPDC ilifungua Akaunti tatu za Esrow baada ya Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  kutoa idhini kufunguliwa kwa akaunti kwenye Benki ya Stanbic, ikiwa ni moja ya masharti yaliyowekwa na mkopeshaji ili  kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya gesi asilia, kutoka Benki ya Exim ya China. Mkopeshaji alipendekeza Akaunti hizo zifunguliwe kwenye benki ya Stanbic na ambapo taratibu za manunuzi zilizingatiwa, ikiwemo ushindanishaji wa watoa huduma.

 Akaunti hizo tatu zilizofunguliwa ni pamoja na:
1. Akaunti ya Mapato ya Gesi 
Lengo la akaunti hii ni hifadhi mapato yote yatakayo tokana na mauzo ya gesi kwa njia ya bomba jipya.

2. Akaunti ya Uendeshaji 
Akaunti hii ina jukumu la kuhifadhi fedha zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa mradi wa miundombinu hiyo mipya ya gesi asilia.

3. Akaunti ya Kulipia Deni
Akaunti hii imefunguliwa kwa ajili ya kulipa madeni yatokanayo na mkopo.

Akaunti hizi zinadhibitiwa na masharti yaliyowekwa kwenye makubaliano (Mkataba) ya Menejimenti ya Akaunti hizo yaliyosainiwa kati ya Benki ya Stanbic (kama Benki ), TPDC (kama mtumiaji wa mwisho), Benki ya Exim ya China (kama Wakopeshaji) na Wizara ya Fedha (kama mdeni kwa niaba ya Serikali ya Tanzania).

TPDC inapenda kuufahamisha umma kwamba, baada ya taratibu zote hizo kufuatwa, si sahihi kuuhusisha mchakato huu na tuhuma zozote na ukiukwaji wa sheria za nchi. Aidha, ifahamike kwamba Akaunti ya ESCROW ni akaunti ya kawaida kabisa katika utekelezaji wa miradi kama huu wa gesi asilia.

TPDC Kwa Maendeleo ya Taifa!
Imetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji- TPDC
S.L.P 2774
Dar Es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2016

    Ndiyomnazidi kuwachanganya wadau iwe wasomaji wa mitandao na pia waandishi wa habari kwa taarifa isiyo ya kina.

    Taarifa ingeanza kwa kufafanua kuwa neon ESCROW ni neno la kitaalamu katk fani ya uhasibu na taasisi za fedha. Ni kama kutumia neon la taaluma ya kitabibu kusema neon Sickle cell.

    Escrow hivyo ni neno la aina ya akaunti maalum inayofunguliwa kufanikisha mradi au jambo maalum ktk fani ya uhasibu na utawala wa fedha (financial/banking management).

    Hivyo wananchi wataendelea kusikia mfano kesho serrikali ikafungua akaunti ya ESCROW ''B'', siku nyingine akaunti ya ESCROW ''Z'' n.k
    Hivyo wanachi wasiwe na wasiwasi na neon ESCROW bali tu waulize dhumuni la kufungua mfano akauti ya TPDC ESCROW ''Y'' ni nini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...