Na  Bashir  Yakub.

Uhaini  ni  kosa  la  jinai .  Ni  kosa  kati  ya  makosa  makubwa  ya  jinai.  Katika  jinai  yapo  makosa  makubwa  na  yapo  makosa  madogo.  Yumkini  udogo  na  ukubwa    wa  kosa  waweza  kupimwa  kwa   kutizama  adhabu  ya  kosa.  Kosa  ambalo  huadhibiwa  kwa  adhabu  ndogo   huwa  ni  kosa  dogo  na  lile  ambalo  huadhibiwa  kwa  adhabu  kubwa  huwa   ni  kosa  kubwa.

1.NI  SHERIA  IPI  HUELEZA  MAKOSA  YA  JINAI.
Sheria  zinazofafanua  makosa  ya  jinai  zipo  nyingi.  Hakuna  sheria  moja  katika  makosa  ya  jinai.  Hata  hivyo  sheria  kuu  katika  makosa  ya  jinai ipo.  Ni  sheria  inayojulikana  kama  kanuni  za  adhabu( penal  code).  Hii  ni  sheria  kuu  katika  makosa  ya  jinai.  

Ni  sheria  inayoeleza  karibia  makosa  yote ya  jinai.  Mbali   na  sheria  hiyo  pia  zipo  sheria nyingine kama  za  kuzuia  na  kupambana  na  rushwa, sheria  ya  uhujumu  uchumi, sheria  ya  ugaidi na  nyinginezo.  Hizi  nazo hueleza  makosa  ya  jinai.  

Tofauti  kubwa  kati ya sheria  hizi  na  ile  ya  kanuni  za  adhabu  ni kuwa  hizi  sheria  nyinginezo  hueleza  makosa  rasmi  ya  jinai. Kwa  mfano  sheria  ya  ugaidi  itaeleza  mambo  ya  ugaidi  tu  na  si vinginevyo,  sheria  ya  uhujumu  uchumi  itaeleza  makosa  yanayotokana  na  uchumi  tu  na  si vinginevyo,  sheria  ya  utakatishaji  fedha  itaeleza  utakatishaji  fedha  tu  na  si  vinginevyo. 

 Wakati  sheria  ya  kanuni  za  adhabu  ndani  mwake  utakuta  makosa  tofauti  tofauti  ya  jinai.  Utakuta  makosa ambayo  hayafanani na yasiyokuwa na  uhusiano. 

Utakuta  kuhusu  kubaka,  kuiba, kupigana, kuua, kuharibu  mali, rushwa, kughushi ,  uhaini  na  mengine  mengi. Kwahiyo  kwa  mtu anayehitaji  kuyajua  makosa  ya  jinai  basi na  asome  sheria  ya  kanuni  za  adhabu.

KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...