Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St.Joseph jijini Dar es Salaam,Aisha Ramadhan,akiumiliki mpira wakati timu yake ilipopambana na timu ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Memorial hapo jana katika bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania, lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya jijini Dar es Salaam,wakimkimbiza kuku wakati wa bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
John Mwakipesile ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam,akiruka juu kujaribu kumtoka beki wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Abbakari Omary wakati timu hizo zilipomenyana hapo jana na kutoka suluhu ya bila kufungana katika bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania,lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...