Mhandisi mitambo wa Azam TV, (kushoto), akiwapatia maelezo ya juu ya chumba cha uthibiti matangazo, (control room), wabunge wa EALA-Tanzania walipotembelea studio za Televisheni hiyo, Tabata jijini Dar es Salaam, Aprili 22, 2016.
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WABUNGE
wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania, wamewafagilia
wafanyabiashara wakubwa hapa nchini, Dkt. Reginald Mengi na Mzee Said Salim
Bakhresa, kwa uthubutu wao wa kutambua na kuzitumia fursa zilizopo kwenye Jumuiya
ya Afrika Mashariki na kuwahimiza watanzania wengi kuiga mfano huo.
Pongezi
hizo walizitoa Aprili 22, 2016 wakati walipotembelea studio za Azam Media,
mwishoni mwa ziara yao ya kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la
kuhamasisha umma wa Watanzania kuchangamkia fursa kwenye Jumuiya hiyo ambayo
mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Charles Makongoro Nyerere ameiita kuwa ni jumuiya
ya watu wa Afrika Mashariki na sio ya
viongozi.
“Napenda
kumpongeza sana mzee Said Salim Bakhresa kwa kutambua fursa zilizopo kwenye
Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Azam TV inaonekana kwenye nchi kadhaa
wanachama wa Jumuiya lakini pia bidhaa za Azam zimesambaa karibu Afrika
Mashariki na Kati, na Mzee Mengi pia anastahili pongezi kwa utambuzi wao wa
fursa zilizopo kwenye Jumuiya.” Alisema Mh. Shy-Rose Bhanji, ambaye alikuwa
miongoni mwa wabunge hao.
Kuna
haja ya watanzania kuondokana na dhana ya kujiona wanyonge kwenye Jumuiya hii
kwani wanatakiwa kuchangamkia kila fursa iliopo, mfano mimi ni mwalimu wa
hisabati, ukijumlisha na Kiswahili, unaweza kupata kazi huko Sudani Kusini na
maeneo mengine ya Afrika Mashariki, kwani walimu wa Kiswahili wanahitajika
sana, unachopaswa ni kujiongeza tu, unakuwa na kitu kingine cha ziada.” Alisema
Mh. Nderaikindo Kessy.
Kwa
upande wake, Mh. Abdulla Mwinyi, alisema, wabunge wa EALA kutoka Tanzania,
wamefanya jitihada hizo za kutembelea vyombo vya habari kwa kutambua mchango
mkubwa unaotolewa na waandishi wa habari katika kuhabarisha umma na vyombo vya
habari vinao mchango mkubwa wa kutangaza kwa kina fursa za kiuchumi kwenye
Jumuiya.
Akitoa
taarifa ya utendaji kazi wa kituo cha televisheni cha Azam TV, Mkurugenzi wa
uendeshaji vipindi wa Azam TV, Yahya
Mohammed alisema, malengo ya Azam TV ni kufika kufanya kazi zake kwenye nchi
zote za Afrika Mashariki, na Kati, ambapo kwa sasa wana soko zuri tu DRC,
Rwanda, Uganda. Kenya na Burundi zinajikongoja lakini matumaini makubwa ya
kulishika soko la nchi hizo yapo.
Mh. Shy-Rose Bhanji, (kulia), na Mkuruenzi wa TV, Bi. Jane Shirima
Mkuu wa chumba cha habari Azam TV, Bw. Hassan Mhelela, akizungumza wakati wabunge hao (hawapo pichani), walipotembelea chumba cha habari







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...