Kutoka kushoto ni DariaMwakaramba kutoka Tanzania, Asya Idarous Khamsin toka Tanzania/Houston na Flora toka North Carolina ambao siku ya Ijumaa April 29, 2016 wataitikisa kongamano la DICOTA 2016 jijini Dallas kwa vivazi vya kukata na shoka kutoka Tanzania na hapa Marekani.
Kulia ni Mhe. Balozi Wilson Masilingi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na mkewe Marystela Masilingi (Wanne toka kushoto) wakimkaribisha Balozi Anisa Mbega  (wapili toka kushoto) anayeshughulikia maswala ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa siku ya Alhamisi April 28, 2016 katika hotel ya Hyatt Regency ambako ndiko litakapofanyika Kongamano la DICOTA 2016 kuanzia siku ya Ijumaa April 29, 2016.
Kutoka kushoto ni Nasibu Sareva, Fredrick Mjema, Asha Nyang'anyi, Balozi Anisa Mbega, Mohamed Nuh mwakilishi wa People's Bank of Zanzibar, Emmanuel Kimaryo mwakilishi kutoka CRDB na Lunda Asumani wakiwasili katika hotel ya Hyatt Regency siku ya Alhamisi April 28, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...