Mgombea wa Nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Igor Luksic ( Montenegro), akimwaga sera zake mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakati wa majadiliano/mhadalo usio rasmi ulioandaliwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lengo kutoa fursa kwa wanaowania nafasi ya Katibu mkuu kueleza sera zao na kisha kuulizwa maswali
Bi. Irina Bokova ( Burgalia) mmoja wa wanawake wanne waliojitokeza hadi sasa kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa naye akijieleza mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Bw. Antonio Guterres ( Portugal) mmoja wa wagombea waliohojiwa katika siku ya kwanza ya mdahalo usio rasmi wa kuwasikiliza wagombea waliojitokeza kuwaania nafasi itakayoachwa wazi na Ban Ki Moon, mwishoni mwa mwaka huu. jumla ya wagombe tisa wamekwisha jitokeza mpaka jana ( jumanne).
Taswira ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika siku ya kwanza ya mdahalo wa kihistoria ya wagombea nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mdahalo/majadiliano ya kwanza ya aina yake kufanyika katika nafasi ya kumtafuta Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa .
Na Mwandishi Maalum, New York
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jana ( Jumanne) limeandika historia kwa mara nyingine, kwa kuanza mchakato usio rasmi wa kuwasikiliza na kuwauliza maswali wagombea watarajiwa waliojitokeza kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mchakato huo ulianza kwa kuwasikiliza wagombea watatu kati ya tisa wakiwamo wanawake wake wanne ambao hadi siku ya jumanne walikuwa wametangazwa rasmi kuwania nafasi hiyo itakayo achwa wazi na Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki Moon anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu.
Katika awamu ya hiyo ya kwanza, kila mgombea mtarajiwa alipewa fursa ya kujieleza na kuelezea visheni yake, sera, mipango, vipaumbele vyake na nini anatarajia kukifanya endapo atachaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Umoja wenye wanachama 193.
Walioshiriki mdahalo huo katika siku ya kwanza walikuwa ni Dr. Igor Luksic ( Motenegro), Bi. Irina Bokova ( Bulgaria) na Bw. Antonio Guterres ( Portugal)
Wengine ambao wamejitokea kuwania nafasi hiyo ni Dr. Damilo Turk ( Slovenia) Prof.Dr. Vesna Pusic ( Crotia), Bi. Natalia Gherman ( Moldova), Dr. Srgian Kerim ( Macedonia), Bi. Helen Clark ( New Zeland) na Bw. Vuk Jeremic ( Serbia)
Ulikuwa ni mdahalo wa aina yake wa kwanza kutokea tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa miaka karibu 70 iliyopita, mdahalo ulioendedeshwa katika mazingira ya uwazi, na ambao kwayo umebadilisha kabisa utaratibu wa kumpata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...