Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wakufunzi wa mafunzo ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Athuman Libanda baada ya kuhitimu mafunzo ya siku 12 ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kumalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kuwafundisha vijana wanaojiunga na jeshi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Bregedia Jenerali, Michael Isamuhayo, Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’i Issa (nguo nyekundu) na viongozi wengine wa jeshi hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, .Jenista Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wakufunzi wa mafunzo ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Bi. Joyce Shauza baada ya kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali ya siku 12 yaliyoendeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kumalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kuwafundisha vijana wanaojiunga na jeshi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Bregedia Jenerali, Michael Isamuhayo, Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa (nguo nyekundu) na viongozi wengine wa jeshi hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) akiondoka katika ukumbi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mara baada ya kufunga mafunzo ya siku 12 ya wakufunzi wa somo la ujasiriamali mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali, Michael Isamuhayo. Mafunzo hayo yaliendeshwa na NEEC.
Na Mwandishi wetu.
Jumla ya wakufunzi 53 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali na kutunukiwa vyeti.
Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa muda wa siku 12 na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Mafunzo hayo yalifanyika katika kambi ya Mgulani na kuhusisha mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Pwani.
Akikabidhi vyeti hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira Vijana na Walemavu,Bi.Jenista Mhagama alisema wakufunzi hao wana wajibu wa kuwafundisha somo la ujasirimali vijana wanaojiunga na jeshi hilo ili kupambana na tatizo la ajira nchini.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...