WAZIRI wa maji Mhandisi Gerson Lwenge (pichani) ameombwa kuingilia kati na kushughulikia kwa haraka utata uliogubika utekelezaji wa mradi wa Bwawa la maji la malezi lilipo kata ya Malezi ,Mjini Handeni ambao haujaanza licha ya Benki ya Dunia kutoa shs. 740 kwa ajili ya mradi huo.

Wakizungumza katika mahojiano na wawakilishi wa vyombo vya habari waliokuwa wanafuatilia utekelezaji wa mradi huo, wakazi hao ambao wanalazimika kutembea kilometa zaidi ya 5 kufuatilia maji katika vyanzo vya maji wamesema hawaoni sababau ya mradi huo kutokuanza licha ya fedha hizo kutolewa.

Kitombo alisema kwa taarifa alizonazo mwaka 2013 Benki ya Dunia iliingiza sh. Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo ambao unatarajiwa uwanufaishe Wakazi Zaidi ya 6000. Gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni sh. Milioni 880. 

Aliendelea kueleza kuwa mwaka jana sh. Milioni 300 zilliingizwa katika akaunti na kufanya jumla ya fedha zilizoingizwa kaikamakauntinkuwa shs. Milioni 700

Pia alieleza mshangao wake kwa nini mradi huo bado unaendelea kutekelezwa na Halmshauri ya Wilaya wakati ambapo eneo la mradi liko Halmashauri ya Mji.

Naye Afisa Mtendaji wa Kata hiyoya Malezi. Muhaji Ramadhani Mlaki alisema kuwa mara nyingi ammepokea wataalamu ambao wanakuja kuona eneo lakini hakuna kinachoendelea baada ya hapo licha ya kuwaambia watu wenye maeneo yao ambayo yameingizw kwenye mradi huo waache kulima.

“Tunapata lawama kwa wananchi kwa sababu tunawalewesha hadi mwisho wanatuambia kuwa na sisi tumekuwa wanasiasa,” alisema.

Naye Cecilia Ibrahimu wa Malezi Kwedinguzo ambaye ana shamba kwenye eneo hilo la mradi wa bwawa alikubali kutoa eneo lake kwa sababu maji ni kero inayowagusa watu wote.

“Sina cha kusema nataka maji tu. Cha ajabu tuliambiwa tutapewa mashamba na kusaidiwa kulimiwa lakini mpaka sasa hatujaonyeshwa mashamba na mradi haujaanza,’ alisema Bi. Cecilia.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata hiyo, Mzee Abdallah Kombo walipoingia katika uongozi kilio ni hicho hicho hadi hivi sasa. Alisema kuwa wananchi wanategemea malambo madogo yaliyochimbwa kwa juhudi za Mbunge wa zamani wa Handeni, marehemu Abdallah Kigoda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inasikititsha sana kuona Misaada ya huduma kwa jamii inatolewa na wafadhili Lakini haifanyiwi kazi ipasavyo.Matokeo yake mradi unakuja kuanza wakati gharama zinakuwa zimepanda na kujikuta mradi unaishia njiani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...