AccessBank yaendelea kuwakumbusha wateja kuweka fedha kwenye akaunti zao za”RAHISI inayowezeshwa na AccessMobile” na kisha wafanye miamala mingi ili waokoe muda na pesa zao.Sambamba na hilo, pindi mteja afanyapo miamala mingi, unaweza kujishindia simu mpya ya kisasa”brand new smart phone”.
Mr Amos Masunga (mmoja wa wateja ambao wamewahi kujishindia zawadi ya simu mpya na ya kisasa), akipongezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa AccessBank Tanzania, Mr. Roland Coulon.
Pichani (kushoto) ni mmoja wa wateja ambao wamewahi kujishindia zawadi ya simu mpya na ya kisasa aina ya Huawei P8 kwa kufanya miamala mingi zaidi kupitia huduma maridhawa ya “RAHISI inayoweshwa na AccessMobile.

Akitoa maoni juu ya hili, Meneja Masoko wa AccessBank, Bw. Muganyizi Bisheko, alisema kuwa, “inafurahisha sana kuona huduma hii inafanya vizuri na imeweza kukidhi kisawa sawa mahitaji ya wateja. tutaendelea kuwaweka wateja wetu mbele na kuwazadia kwa uzalendo wao na uaminifu wao katika kutumia huduma zetu.” 

“Ningependa kuwashauri wateja waendelee kutumia mfumo wetu wa bure wa huduma za kibenki kwa njia ya simu, wafanye miamala mingi na wawashauri ndugu na jamaa kujiunga na mfumo huu kwa kutembelea tawi lolote la AccessBank huu ili nao waweze kufurahia miamala ya bure na kufuzu kwenye mfumo huu wa zawadi.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...