Teresia Mhagama na Asteria Muhozya
Imeelezwa kuwa, Wizara ya Nishati na Madini imeendelea kurahisisha utoaji wa huduma za leseni za madini ambapo sasa wamiliki wa Leseni hizo wanaweza kupata taarifa za ada ya leseni kwa njia ya ujumbe wa simu (SMS).
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza alisema kuwa ili mteja aweze kupata huduma hiyo anatakiwa kuandika neno MEM, ache nafasi , kisha aandike Namba ya Leseni na kutuma kwenda 15341.
Fungameza alisema kuwa hizo ni habari njema kwa wamiliki wa leseni kwani sasa wataweza kupata taarifa hizo kwa wakati na hivyo kulipia ada za leseni hizo kwa wakati.
Aidha Fungameza alisema kuwa Wizara imekuwa ikibuni njia mbalimbali ili kuhakikisha kuwa huduma za utoaji wa leseni za madini pamoja na taarifa mbalimbali kuhusu leseni hizo zinapatikana kwa urahisi na uharaka tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...