Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (katikati) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka. Wengine ni  Afisa Mwandamizi wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (kulia), Meneja Masoko wa benki hiyo, Bw Abdulrahman Nkondo, (kushoto) na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde (wa pili kushoto)

BENKI ya Exim Tanzania imetangaza kupata faida ya sh. bilioni 53. (kabla ya kodi) kwa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka mwaka 2016, sambamba na faida ya kuuza hisa ilizowekeza (capital gain) ya Tsh bilioni 45 mafanikio yanayotajwa kusababishwa na ufanisi wa benki hiyo katika usimamizi mizania.

Aidha, mapato yatokanayo na uendeshaji wa benki hiyo yaliongezeka na kufikia kiasi cha Tsh bilioni 8.4 yakiakisi ukuaji wa asilimia 67 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita.

“Kasi ya mafanikio tuliyomaliza nayo mwaka uliopita ndio tulianza nayo na ndio siri kubwa ya mafanikio haya,’’ alisema Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw Selemani Ponda alipokuwa akitoa ripoti ya awali (kabla ya ukaguzi) ya benki hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Alisema ongezeko hilo lilipatikana kupitia mchanganyiko linganifu baina ya mapato yatokanayo na faida pamoja na yale yasiyotokana na faida.

Kwa mujibu wa Bw. Ponda katika kipindi hicho faida kwenye riba ilikuwa kwa asilimia 24 na kufika sh. Bilioni 21 ikilinganishwa na kiasi cha sh. 17 kilichopatikana katika kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita. Ongezeko hilo limechagizwa na mkazo wa benki hiyo katika amana za gharama nafuu, wingi wa matawi ya yapatayo 45 ya benki hiyo pamoja na usimamizi mzuri wa mizania.

Zaidi, tozo mbalimbali za huduma za kibenki katika kipindi cha mwaka ulioipita kiliongezeka kwa asilimia 21 hadi kufikia sh bilioni 9, kutoka kiasi cha sh bilioni 7.5 kilichopatikana mwaka uliopita.

“Ongezeko hilo pia lilichagizwa na faida katika biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni ambayo mapato yake yaliongezeka kwa asilimia 11 na kufikia kiasi cha Tsh bilioni 2.5 sambamba na mapato mengine ya ada kutokana na ufanisi katika utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.,’’ alifafanua.

Alisema matumizi ya benki hiyo yalliongezeka kwa asilimia 35 kutokana na mabadiliko inayopitia kupitia uwekezaji mkubwa kwenye rasilimali watu, michakato mbalimbali pamoja na teknolojia.

“ Miradi mingi ya kiteknolojia inatarajia kukamilika kwenye robo ya tatu ya mwaka huu.,’’ alibainisha Bw Ponda.

Akizungumzia upanuzi wa benki hiyo iliyoufanya nchini Uganda alisema rasilimali za benki ya Exim zimeweza kukua kwa asilimia 14.63 katika kipindi cha robo ya mwaka huu na hivyo kufikia kiasi cha Tsh Trilioni 1.44 ilinganishwa na kiasi cha Tsh Trilioni 1.25 kilichorekodiwa mwishoni mwa mwaka uliopita.

“Exim tunaahidi kuendelea na muelekeo huu ulio sahihi kwetu na kwa wateja wetu katika kutimiza malengo yetu. Ripoti hii inaonyesha kuwa robo ya kwanza ya mwaka huu ilikuwa na mafanikio makubwa na ya kujivunia,’’ alisema Bw Ponda huku akiwapongeza wafanyakazi na wadau wote waliochangia mafanikio hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...