Na Lilian Lundo – Maelezo

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limeazimia kuongeza idadi ya madampo na kurekebisha miundombinu ya dampo la Pugu ili kuhakikisha jiji linakuwa safi.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita alisema Baraza hilo limeazimia kuongeza na kurekebisha miundombinu baada ya ziara walioifanya na kugundua mapungufu katika dampo la Pugu.

“Tumegundua kuna udhaifu mkubwa katika dampo la Pugu, magari yanayopeleka taka yananasa barabarani hivyo tukaona kuna sababu ya kutengeneza miundombinu, hivyo tumetenga milioni 700 kwenye bajeti hii ili kutengeneza barabara hiyo,”alisema Mhe. Mwita.

Aidha, alisema kwamba baraza limetenga kiasi cha shilingi milioni 200 katika bajeti ya 2016/17 ili kununua eneo Mkuranga kwa ajili ya dampo, huku wakiendelea na mchakato wa kuongeza madampo mengine Kigamboni na Kisarawe ili kuhakikisha taka zote zinazozalishwa ndani ya jiji la Dar es Salaam zinapelekwa kwenye madampo badala ya kuzagaa mitaani.

Kwa upande wake, Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Mussa Kafana alisema kuwa, suluhisho la kumaliza taizo la uchafu si kuwa na dampo tu bali ni kuwepo kwa vifaa maalumu vya kuhifadhi taka. Hivyo baraza likaamua kuwepo na vyombo vya kuhifadhia taka katika mitaa yote ya jiji la Dar es Salaam ili kudhibiti uzagaaji wa taka.

Usafi ni moja ya kipaumbele cha Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo kwa mara ya kwanza alitangaza siku ya Uhuru wa Tanzania (Tisa Desemba) iazimishwe kwa kufanya usafi nchi nzima ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu pamoja na kuiweka Tanzania katika hali ya usafi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...