Wakati tukiendelea kuvisaka na kuvimulika vijipu upele, leo tumekutana na taswira hii ya foleni ya watu wenye utulivu wakisubiri kupanda mabasi ya UDART kistaarabu. Utamaduni huu mpya umetupa furaha na faraja sana. Hongera UDART na hongera Abiria wa Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2016

    Daa kama kijijini vile watu wamepanga foreni ya ugawaji

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2016

    Asanteni sana huo ndio uzalendo na ustaarabu sio kila kitu ubabe ubabe tu ni mimi ndugu yenu The mdudu, nilie huku Uingereza kwenye City ya Leicester ilio shangaza dunia kwa ubingwa wa ligi kuu ya England, ila to be honest mimi huko siludi mpaka MAJIPU yaishe maana Tanzania yetu iliotwa na MAJIPU kila kona

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2016

    Kupanga foleni wala si Sheria, ni uungwana na ustaarabu tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2016

    Hongera DART na utulivu wa watu wetu. Huyo wa Leicester ambaye anaona kwa wenzio ndio maana sana kuliko kwao tunamuombea fanaka kubwa ili siku moja ajaliwe arudi kusaidia kwao. Ujinga wetu ni pale tunapokimbia kwetu na kupadharau tukidhania hao tuliokimbilia kwao wanatuheshimu. Jamaa anasubiri kufa wamchangie kumrudisha makaburini huku anapopaita hapafai! Wabongo wengine ajabu kweli.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2016

    hongera sana wananchi.
    Nchi zote zilizoendela hufanya hivyo. Hakuna mtu kumkatiza aliyekuwa kwenye mstari. Hii ilikuwa inatokea Tanzania tu. Ulaya na Marekani wanapanga foleni ,hata uwe nani unafuata mstari. Ni ustaarabu unaopendeza.Maana binadamu wote nisawa, hakuna aliyebora hasa kwenye huduma za jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...