Mkurugenzi wa Her Initiative Lydia Charles akizungumza na vyombo vya habari

    Her Initiative iliyojulikana mwanzo kama Teen Girls Supportive  Initiative (TGSI) wameandaa mkutano mkubwa ujulikanao kama Panda utaowajumuisha wanafunzi wa kike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari yote katika lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo.
      Her Initiative ni asasi ya wasichana ambapo wao wenyewe ndio mhimili wa maongezi. Her Initiative inawapa wasichana nafasi ya kuwakilisha na kusimamia maswala yao wenyewe ya kiuchumi, elimu, kiutamaduni na kiafya. Zaidi Her Initiative inamjengea uwezo msichana wa kutafuta suluhu ya changamoto zake mwenyewe bila kutegemea watu wengine. Vyote hivi hufanyika kupitia kampeni, matamasha, semina na kuwapa msaada wa mahitaji ya kielimu, kiuchumi na kiafya kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali.
    Panda ni event inayohusu ujasiriamali, uvumbuzi, ubunifu na matumizi mazuri ya pesa. Kama tunavyofahamu, wasichana tuna matumizi mengi ya pesa na mara nyingi matumizi haya huzidi kipato cha pesa tunachokipata. Kwa kuona hili sisi kama wasichana tumeamua kuandaa event hii ili kusaidiana kuepuka hatari zinazoweza kutokana na kutokuwa na uchumi imara. Madhumuni ni kumjengea msichana hali ya kujitegemea kwa kumfundisha namna ya kuhifadhi pesa kupitia benki tofauti na mifuko mbalimbali ya jamii. Pia tunalenga kuwafundisha wasichana walioanza maswala ya ujasiriamali na uvumbuzi namna ya kuimarisha biashara, mawazo ya biashara na taasisi. Vilevilea kuwahamisha wasichana ambao hawajaanza kujishughulisha kuanza kufanya vitu tofauti tofauti vya kujikwamua kiuchumi.
Mkutano huu utafanyika ukumbi wa Theatre One katika Chuo Kiuu cha Dar-es-salaam. Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bona Kalua ndio mgeni rasmi katika shughuli hii. Wageni wengine watakaohudhuria na kutoa maneno ya ushauri kwa wasichana ni pamoja na Ruge Mutahaba, Shekha wa Shear Illusions, Jeniffer Shigoli, Rose Ndauka, Dorice Mollel, Aika Navykenzo na Lemutuz.
     “Sisi ni wasichana na tunaimani kubwa ya kwamba tuna uwezo wa kuwahamasisha wanadada wenzetu kujishughulisha na vitu mbali mbali, kujilinda na vile vile kuleta maendelleo katika jamii kwa ujumla. Uwezo tunao na tunaamini Panda ni mwanzo wa maendeleo mengi zaidi kwa wasichana. Nina wasihi wasichana wajitambue, wajithamini na wachakarike” alisema Lydia Charles ambae ni mkurugenzi mkuu wa Her Initiative.
   Waliounga mkono shughuli hii ni Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kupitia serikali ya wanafunzi chini ya wizara ya jinsia.
   Wadhamini wa shughuli hii ya Panda ni GEPF, Shear Illusions, Vijana Inc na AJ Graphics. Tungependa kutoa shukrani za dhati kwenu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...