Frank Mvungi-MAELEZO
Serikali imewataka wauzaji wa vifaa vya Mawasiliano vya mkononi (mobile devices) kuacha mara moja tabia ya kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’) za vifaa hivyo kwani watakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua milioni 30 au vyote viwili.Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.
“Namba tambulishi (IMEI) za vifaa vyote vya Mawasiliano ya mkononi ambavyo vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo tarehe 16 June 2016. “Aalisema Mungy.
Akizungumazia kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya simu zote zisizokidhi viwango, Mungy alibainisha kuwa idadi ya simu hizo imeshuka kutokana na elimu ambayo wameitoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.Alisema lengo la elimu hiyo kwa umma ni kujenga uwezo kwa wananchi kutambua simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Natambua TCRA inafanyakazi Tanzania yote bara na Zanzibar. Jee huko visiwani Zanzibar mmeshapeleka elimu ya kutosha?
ReplyDelete