JENGO la ghorofa 16 la mtaa wa Indira Ghandi lililokuwa likihatarisha maisha kutokana na kujengwa chini ya viwango.
Kufuaatia agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi la kuvunja jengo hilo, jengo limekamilika kuvunjwa. Jengo hilo limevunjwa kufuatia pia kuanguka kwa jengo lingine lililokuwepo mita chache kutoka katika jengo hilo ambalo pia lilijengwa ghorofa 16 badala ya ghorofa nane. Jengo hilo liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 34, mwaka 2013.
Hivi Karibuni Mhe. Lukuvi aliagiza kubomolewa kwa jengo hilo kufanyike ndani ya siku 90. Hatahivyo zoezi la ubomoaji limefanikiwa kukamilishwa kabla ya siku 50.
Mhe Waziri William Lukuvi akiwa na wataalamu katika ufuatiliaji wa ubomoaji wa Jengo la ghorofa 16 la mtaa wa Indira Ghandi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...