Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza na madaktari wa wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar na nchini Uingereza waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifanya matibabu ya moyo, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Taasisi yake ndio kiungo cha kuunanisha taasisi zilizoshiriki kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo.

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akizungumza hatika hafla ya kufunga kambi ya madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuwaaga madaktari wa nchi hizo.
Picha ya pamoja ya madaktari bingwa wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti za nchi tatu.
Daktari bingwa wa kufanya oparesheni ya BAY PASS kwa watu wenye matatizo ya moyo(Jina lake halijpatikana mara moja) akizungumza katika hafla ya kuwaaga madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam leo.
MADAKTARI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamefunga kambi ya Madaktari wa tiba ya Moyo wa kutoka Saudi Arabia, Uingereza na Qutar na baaadhi ya madaktari wenye utaalam wa tiba ya matatizo ya moyo hapa nchini.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka nchi za Saudi Arabia, Uingereza na Qutar jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa kambi hiyo imejumuisha pamoja taasisi nne kutoka nchi tatu tofauti.
Abri amesema taasisi zilizoshiriki kambi ya Moyo Muhimbili ni Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktari kutoka Saudi Arabia, Taasisi ya Araf kutoka Qutar na taasisi ya Dhi Nureyn ya hapa nchini na Taasisi ya Jakaya Kikwete.
Amesema kuwa kambi hii ya sasa imefanikiwa kuwatibu watoto wenye matatizo ya moyo 66 ambao walikuwa wamepangwa kusafirishwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu sasa wametibiwa hapa nchini na kuokoa mabilioni ya fedha za serikali.
Kwaupande wake Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala amewashukuru madaktari kutoka taasasisi hizo kwa kuja hapa nchini na kuokoa watoto wenye matatizo ya moyo 200 ambao wametibiwa hapahapa nchini.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...