Ni miaka mitatu imepita tangu ulipotwaliwa Mpendwa Mama
yetu Victoria. Ni Roho Mtakatifu pekee anayetufariji kila mara majonzi
na huzuni vinapotujaa mioyoni. Tunaamini kuwa Mama umepumzika katika
utukufu wake Mungu.
Unakumbukwa sana na mumeo Thomas Kiama, wanao Evelyn, Grace, Mary, Agnes, Esther na Stella,wakwe zako Wilfred, Noel na Richard, wajukuu zako Clifford, Ian, William, Eleon, Mainda, Kandi, Agness, Mboni, Lincoln na Lucas.
Upendo, ucheshi, ukarimu na tabasamu lako vitabaki kuwa nguzo katika maisha yetu siku zote.Kipenzi Mama tulikupenda sana lakini Mungu Mwenyezi alikupenda zaidi. Umepumzika kwa amani!
Familia ya Thomas M. Kiama
Rest In Peace Mama Victoria T. Kiama. Wewe umetangulia nasi sote kwa Muumba ni marejeo yetu.
ReplyDeleteMfuo wa hicho Kidani ni wa zamani kweli kweli, yaani pia umenikumbusha Marehem Mama yangu (Rest In Peace).