Na Bashir
Yakub
Sheria ya Ajira
na Mahusiano Kazini
ya 2004 ndiyo sheria mama
katika masuala ya
ajira. Kwa anayetaka kujua
haki na wajibu
wa kazi na mfanyakazi,
mwajiri na mwajiriwa
basi na asome
sheria hii. Sheria
hii ilianza kutumika rasmi tarehe
5/ 1/ 2007.
Misingi mikuu ya sheria
hii ni usawa
wa ajira kwa jinsia, ujira
unaolingana na kazi inayofanywa
na mfanyakazi, haki na
maslahi bora kwa
mfanyakazi, mazingira bora na
salama ya kazi
na mengine mengi
hasa yanayoshabihiana na
haki za binadamu.
Kumwachisha kazi mfanyakazi
ni moja ya
maeneo muhimu katika
sheria hii. Wakati gani
mfanyakazi aachishwe kazi, kwa
kosa gani, utaratibu wa kumwachisha
kazi, stahiki zake
baada ya kuachishwa
kazi, uachishwaji kazi
haramu, utaratibu wa hatua
za kuchukua panapo
uharamu katika kuachishwa
kazi ni sehemu ya
mambo muhimu katika
sheria hii.
Makala haya yataeleza
habari hii ya kuachishwa
kazi lakini yatalenga
kipengele kimoja tu
cha uhalali wa kumwachisha
mfanyakazi kwa kosa la
kwanza.
1.NI IPI
TAFSIRI YA KUACHISHWA
KAZI.
Kuachishwa kazi ni
hatua ambapo muajiri
husitisha mkataba wa
ajira kwa notisi
au bila notisi
kwasababu mbalimbali zikiwemo
za utovu wa nidhamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...