Shule ya Msingi Ulonge iliyopo katika Manispaa ya Iringa takriban kilometa 10 kutoka Iringa Mjini, imepokea jumla ya madawati 30 kutoka kwa mdau wa maendeleo Bw.Suhail Ismail Thakore (pichani kulia) wa Manispaa ya Iringa.
Awali shule ilikuwa na uhitaji Wa madawati 37, hivyo baada ya kupokea madawati hayo, mahitaji yatakuwa 7. Na baada ya kuwepo madawati 6 mabovu ambapo yakikarabatiwa hayo 6 uhitaji Utakuwa ni dawati moja.
Thamani ya madawati hayo 30 ni shilingi 1,800,000/-.Shule ya Ulonge ina jumla ya wanafunzi 495 walimu 9.
Sehemu ya madawati yaliyotolewa na mdau wa maendeleo Bw.Suhail Ismail Thakore
Mdau wa maendeleo Bw.Suhail Ismail Thakore wa Manispaa ya Iringa akiwa na walimu wa shule hiyo baada ya kutoa msaada wa madawati hayo 30.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...