Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Aprili 2016 leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja.Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 umepungua hadi asilimia  5.1  kutoka asilimia 5.4.
 Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja akifafanua  jambo  kwa waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania.kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu, ya Jamii). 

Na. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
OFISI ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 na kusema kuwa umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwepo mwezi Machi, 2016.

Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Aprili 2016 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Machi mwaka huu.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo ametoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam na kueleza kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema Takwimu zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwenye bidhaa zinazotumika kupima mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2016 zimeainisha kuwa bidhaa zisizo za vyakula katika soko zikiwemo Gesi , dizeli na mafuta ya taa zimechangia kupungua kwa mfumuko huo.

Amesema kuwa pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa hizo kwa mwezi Aprili 2016, baadhi ya bidhaa za vyakula ikiwemo mchele, unga wa Mahindi na mkaa ilionyesha kuongezeka katika kipindi hicho.

Akizungumzia Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania kwa mwezi Machi na Aprili Bw. Kwesigabo amesema kuwa zimeongezeka hadi kufikia 102.46 kutoka 101:93 za mwezi Aprili.

Amesema kuwa tofauti na mwezi Machi bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi kwa mwezi Aprili ni unga wa muhogo, dagaa, choroko, maziwa ya ungana na matunda aina ya machungwa.

Aidha,bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mvinyo, bia kuni na mazulia.

Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Aprili, 2016 umefikia shilingi 97 na senti 60 ikilinganishwa na uwezo wa shilingi 98 na senti 11  wa mwezi Machi 2016.

“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Aprili 2016 umepungua, hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza  ya shilingi 2.40 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Machi " Amesema Kwesigabo.

Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki mwezi Machi, 2016, Kwesigabo amesema una mwelekeo unaofanana; Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.27 kutoka 6.45 huku Uganda ukifikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 6.2 zIlizokuwepo mwezi Machi 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2016

    Tusikate tamaa. Mambo yatakwenda sawa. Hebu soma hii hapa:
    The fastest growing economies in Africa by GDP growth rate, as projected by IMF for 2016, are: Cote D’Ivoire (8.5%), Tanzania (6.9%), Senegal (6.6%), Djibouti (6.5%), Rwanda (6.3%), Kenya (6.0%), Mozambique (6.0%), Central African Republic (5.7%), Sierra Leone (5.3%) and Uganda (5.3%

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2016

    Mara mfumuko wa bei umeongezeka ''kiduchu'' huku ukiterenka toka asilimia 5.4 mpaka 5.1.

    Mkurugenzi na Prof. taarifa yenu labda haijaeleweka kwa waandishi wa habari na sisi wasomaji tunashindwa kuielewa taarifa hii kwa umma.

    Au Je ni uoga Ofisi ya Takwimu ya Tifa wa kuonekana kuwa ni ''wahujumu'' wa ''awamu hii ya tano'' mpaka manahisi msiwe ''majipu'' na kutoa habari inayokinzana ukisoma taarifa hii mstari kwa mstari, ''neno kwa neno''.

    Mwisho mnaombwa ofisi na taasisi zote mnapotoa habari kwa umma zinazohusisha ''data'', statistics a.k.a takwimu mzitoke kama takwimu zinavyosema bila woga ili tuelewa hali hali na pia mtakuwa inaisaidia serikali kujua wapi wafanye vizuri zaidi.

    Mdau
    Mlaji wa Huduma na bidhaa mtaani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2016

    Sio kweli! Tskwimu zao nizauongo;! Mfumuko wa being uko juu sana tofauti na inavyotajwa!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2016

    Ofisi ya Takwimu Taifa fanyeni kazi kitaalamu bila kuingiza siasa.

    Maana taarifa sahihi toka kwenu Ofisi ya Taifa ya Takwimu hutoa dira kwa vyombo vingi vya serikali, Vyuo vya Elimu ya Juu na hata watu wa kawaida kujua wapange vipi mipango yao.

    Kuweni huru kutoa taarifa sahihi zilizokamilika bila utata wowote ili zikisomwa zieleweke kufuatana na hali halisi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2016

    Ukawa tusha kuchokeni kila kitu kwenu kibaya so tokeni mapovu watu mbele kwa mbele #AsanteJPMngomainogile

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...