Mtaalamu kutoka Marekani, Dk Brian McMahon akizungumza na madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuhusu tiba ya homa sugu ya ini inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B. 
Dk Edwin Masue wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwasilisha mada kuhusu dalili za homa sugu ya ini inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B.
Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Na Neema Mwangomo-MNH.
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH-inatarajia kuanza kampeni ya kupima na kutoa tiba kwa  ugonjwa wa Homa Sugu ya Ini ambao  unasababishwa  na Virusi vya  HEPATITIS B .
 
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Edwin  Masue amesema kundi la ndio limeonekana kuathirika zaidi  kwa kuwa mtoto anapata maambukizi kutoka kwa mzazi  .
 
Kwa mujibu wa Dk. Masue mtoto anapozaliwa lazima apatae chanjo,  na pia mama mjamzito ambaye anagundulika kuwa ana Virusi vya HEPATITIS B  hupatiwa dawa ya  kumkinga mtoto katika miezi mitatu ya mwisho kabla ya kujifungua .
“Tuangalie uwezekano ili watu waelewe tatizo hili mapema , wapime na wawahi kupata matibabu kwani maambukizi makubwa yanatoka kwa mama kwenda mtoto  na kwa wale wanaoanza kutumia dawa za VVU wanatakiwa kupima ugonjwa wa homa ya Ini kwa kuwa virusi vinaingiliana,”  amesema Dk . Masue .

Mkakati wa MHN.
Kwa upande wake Daktari John Rwegasha amesema katika kipindi cha Julai mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  kutaanzishwa mradi wa miaka mitano ambao unalenga kupima na kutibu watu ambao watagundulika kuwa na homa sugu ya ini  na kwamba hata baada ya kukamilika kwa mradi huo wananchi wataendelea kupatiwa matibabu bure.

 “ Kuna muongozo wa tiba wa  Shirika la Afya Duniani-WHO- ambao umetolewa mwaka jana hivyo tunataka kuangalia matumizi ya huo muongozo kwenye nchi zetu za Dunia ya tatu , kuna watu wametusaidia tulikuwa hatuna uwezo wa dawa. Awali tulikuwa tunaazima dawa kwenye mradi wa HIV hivyo kupitia mradi huo tutakuwa na dawa pamoja na vitenganishi vya kimaabara,” amesema Dk Rwegasha.

“Kati  ya watu 100, wanane wanatembea na ugonjwa huo bila kufahamu baada ya miaka 20 mtu anapata matatizo ya ini na kusababisha ini kushindwa kufanya kazi na  tumbo kuvimba   hivyo natumia fursa hii kuwaambia wananchi wajitokeze kupima mapema ili waweze kupatiwa  matibabu,” amesema.

Virusi vinavyoenea:
Kwa mujibu wa watalaam , asilimia kubwa ya Virusi vya HEPATITIS B vipo kwenye damu , mbegu za kiume  , ute wa mwanamke na hedhi ya mwanamke  na kwamba  maambukizi yake hayana tofauti na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Dalili za ugonjwa huo:
-Kichefuchefu
-Kukosa hamu ya kula
-Macho kua ya njano
-Mkojo kuwa wa njano
-Kupata choo chenye rangi ya njano ambayo imepauka
-Mwili mzima kuishiwa nguvu.
Hata hivyo dalili hizo si zote zinaenda pamoja , kuna wengine huwa hawana dalili hizo  kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2016


    Muhimbili endelea kuboresha huduma na kuwezesha madaktari wetu kuyatibu magonjwa mengi hapa hapa nchini.

    ReplyDelete
  2. tunashikuru sana kwakutujali nakutaka kutuokowa. ila maomba msambaze huduma hii mikowani mana hatuna uwezo wakuenda Dar ila tunafamu tanaishi na homa ya ini tusaidieni

    ReplyDelete
  3. tanaomba kusogezewa hoduma hii Mbeya mana tayari tulishapima tunaitaji kutibiwa

    ReplyDelete
  4. Nijambojema kuanzisha kampeni ya kuwafikia watu wengi hasa ktk mikusanyiko ya sherehe mbalimbali za kitaifa bila kusahau makanisani na misikitini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...