Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye amemjulia hali Mzee Omary Nyimbile, baba wa
Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile .
Mhe.
Nape ambaye yupo kwenye ziara ya utekelezaji wa ahadi zake jimboni
kwake na kuonana na wananchi alifika kwenye hospitali ya Nyangao
mwishoni mwa wiki iliyopita na kupokelewa na Diwani huyo wa kata ya
Mtama kupitia Chama Cha Chadema.Mheshimiwa Mbunge wa Mtama alimjulia
hali Mzee Omary na kumtakia heri ya kupona haraka.
Kitendo
cha Mhe. Mbunge kumjulia hali baba wa Diwani wa Chadema kimewashangaza
wengi ambao walidhani viongozi hawa hawatoweza kuzungumza kutoka na hali
ilivyokuwa wakati wa uchaguzi.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akimuangalia Mzee Omary Nyimbile, baba wa
Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile aliyelazwa katika
hospitali ya Nyangao.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na Diwani wa kata ya Mtama Bw.
Hassan Omary Nyimbile (CHASEMA) mara baada ya kuwasili kwenye hospitali
ya Nyangao kumjulia hali Baba wa Diwani huyo aliyelazwa hapo. .
Mbunge
wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye akipewa maelezo juu maendeleo ya hali ya Mzee
Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary
Nyimbile (CHADEMA) aliyelazwa katika Hospitali ya Nyangao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...