Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Alois Matei akizungumza na waandishi habari kuhusu mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam utakaogharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 690 ambapo mradi huo unafadhiliwa na Serikali, Benki ya Dunia,Trade Mark East Afrika na DFID, kulia ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka hiyo Bw. Focus Mauki na mwisho Kapteni Abdullah Mwingamno wa TPA Bandari ya Dar es Salaam.
Mhandisi Mkuu wa TPA, Mhandisi Mary Mhayaya akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa Flow meter mpya ya Kigamboni ambao umeshakamilika na hivyo kuwezesha mafuta yote yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kupimwa na kujulikana kiasi halisi kilichoingizwa hapa nchini ili kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki ikiwemo kodi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Alois Matei akiwa na Baadhi ya wadau wa TPA wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na vyombo vya Habari
leo jijini Dar es Salaam ukilenga kueleza mikakati ya kuboresha miundombinu ya
Bandari hiyo ili kuongeza uwezo wa kupokea mizigo hadi kufikia tani milioni 38
ifikapo mwaka 2030.
(Picha na
Frank Mvungi-MAELEZO)
Jovina
Bujulu -Maelezo
Serikali
imepanga kutumia dola milioni 690 kuimarisha miundombinu ya Bandari ya Dar es
Salaam ili kuongeza uwezo wa kupokea mizigo hadi kufikia tani milioni 38
ifikapo 2030 kutoka tani milioni 16 za mwaka 2014/15.
Akifafanua
kuhusu utekelezaji wa mradi huo wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo
jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
Injinia Alois Matei amesema mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana na Benki ya
Dunia,Trade Mark East Africa na DFID na
unatarajia kuanza kabla ya mwisho wa
mwaka 2016.
“
Serikali,Benki ya Dunia,Trade Mark East Africa na DFID zimetiliana saini makubaliano
ya ushirikiano wa utekelezaji wa mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es
Salaam” alisisitiza Matei.
Akizungumazia
maeneo yatakayohusika katika maboresho hayo Injinia Matei amesema kuwa
yatahusisha uboreshaji na uongezaji wa kina kufikia mita 14 katika gati namba 1
hadi 7 ili kuwezesha meli kubwa zaidi kutia nanga.
Maeneo
mengine ni ujenzi wa gati mpya ya kushushia magari katika eneo la Gerezani
Creek, uchimbaji ili kuongeza kina cha lango la kuingilia meli hadi kufikia
mita 14 pamoja na sehemu ya kugeuzia meli.
Eneo
jingine ni uhamishaji wa gati la mafuta
la Koj pamoja na bomba la mafuta katika eneo la ujenzi, uboreshaji wa mtandao
wa reli ndani ya bandari na ujenzi wa sehemu ya kupakilia na kushushia mizigo.
Ukuaji wa
kiasi cha Shehena ya mizigo inayopita katika Bandari ya Dar es Salaam katika
kipindi cha miaka 5 iliyopita imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 9
kila mwaka huku shehena ya mafuta na makontena ikiongezeka kwa kasi zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...