Timu ya wataalamu kutoka shirika la ndege la Etihad leo wametembelea abiria tisa waliolazwa baada ya Ndege aina ya EY474 ya shirika hilo kupatwa na msukosuko mkali katika anga la wazi ambapo walitoa huduma endelevu, ushirikiano na msaada.
Vile vile walikutana na wanafamilia kadhaa wa majeruhi na kuthibitisha kuwa shirika la ndege la Etihad litagharamia gharama zote za matibabu.
Kati ya majeruhi tisa ambao walikuwa wamelazwa, wengi wao wataruhusiwa kuondoka leo. Rais wa shirika la ndege la Etihad na Mkurugenzi Mkuu Bwana James Hogan amesema: “Rubani wetu na wafanyakazi wa ndege wanapaswa kupongezwa sana kwa utulivu wao na namna ambavyo walishughulikia tukio hili la aina yake kwa utaalamu mkubwa, na huduma waliyoionesha kwa abiria japo kuwa wengi wao walikuwa wamejeruhiwa. Ni ushahidi wa mafunzo ya kiwango cha juu yanayotolewa kwa wafanyakazi wetu ndio sababu athari za msukosuko ulipunguzwa. Wakati huo hakuna kabisa usalama wa ndege,abiria au wafanyakazi walioathirika.”
Shirika la ndege la Etihad linashirikiana kikamilifu na Mamlaka za Indonesia katika uchunguzi wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...