Kwa niaba ya mama yetu mpendwa Mh Dkt Rehema Nchimbi tunapenda kutoa shukrani zetu za upendo kwa Madaktari na wauguzi wote wa Hospitali ya Tumbi Kibaha Pwani  kwa kumtibu vyema mama yetu kipindi chote alipo lazwa hospitalini hapo akiwa anauguza jerahaa lililotokana na kukatwa na kioo kichwani, katika ajali aliyopata hivi karibuni Chalinze, Mkoani Pwani.

Tunapenda pia kuishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na viongozi kwa kumpatia mama yetu huduma kipindi chote alicho lazwa hospitalini hapo, kipekee kabisa tunaishukuru familia ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh Eng: Evarist Ndikilo, dereva wa Mkuu wa Mkoa Njombe, Bw. Mbunda na Katibu wa Mkuu wa Mkoa Njombe, Bw. Ngalupela kwa kusimama kama sehemu ya familia yetu katika kuhakikisha mama yetu anapata huduma zote muhimu.

Shukrani zetu za upendo ziwafikie Viongozi wa CCM taifa na Mkoa wa Pwani, Viongozi wa dini Mkoa wa Pwani Uongozi wa Mkoa wa Njombe, ndugu na marafiki, na wale wote walio mtembelea mama Hospitali ili kumjulia hali na wanaoendelea Kumwombea Mama yetu ili apone kwa haraka.

Mama yetu kwa sasa anaendelea vizuri hivyo tunapenda kuwaondoa wasiwasi wanachi wa Njombe na watanzania kwa ujumla juu ya afya ya mama yetu kwa sasa. Tuzidi kumwombea apone kwa haraka. Tunaomba upendo mliouonesha kwa mama yetu uzidi kudumu na kurithiwa na vizazi vijavyo.

Mama yetu amepata jeraha, baada ya kuchanwa na kioo cha mlango wa moja ya maduka makubwa Chalinze alipo simama kwa mapumziko akiwa safarini kurudi kazini kwake Mkoa wa Njombe tarehe 7 Mei 2016 akitokea Dar es Salaa kikazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...