VIINGILIO MECHI YA YANGA V/S ESPERANCA
Uongozi
wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi yote muhimu
ya mchezo dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola wa kufuzu hatua ya
makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.
Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.
Fuata link chini kwa taarifa zaidi
FIFA YAILIMA FAINI SIMBA, YAPANGA KUISHUSHA DARAJA
Shirikisho
la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi
(sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa
hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro
(Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo.
Kamati
ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis
ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa
kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la
mchezaji huyo, raia wa Kenya.
Fuata link chini kwa taarifa zaidi
VIINGILIO MECHI YA YANGA, ESPERANCE
Uongozi
wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi yote muhimu
ya mchezo dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola wa kufuzu hatua ya
makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.
UWAKILISHI WA NCHI KIMATAIFA
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) lingependa kutoa ufafanuzi kuwa iwapo Bingwa wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu 2015/16 inayoendelea
atashinda pia taji katika fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama
Azam Sports Federation Cup (ASFC), ndiye atayeiwakilisha nchi katika
michuano ya Ligi ya mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.Kwa
msingi huo, timu ambayo itafungwa katika fainali hizo za Kombe la
Shirikisho –ASFC linalodhaminiwa na kituo cha Televisheni cha Azam,
ndiyo itakayowakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho
Barani Afrika katika msimu wa 2016/17
Fuata link hapo chini kwa taarifa zaidi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...